Jumamosi, 6 Januari 2018

MBUNGE WA CHALINZE MH. RIDHIWANI KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA HANDOGO CHALINZE

Posted by Esta Malibiche on DEC 6,2018 IN NEWS

TANZIA 
Jana Tarehe 5 Januari 2017 Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Rhidhiwani Kikwete ameshiriki Ibada ya Msiba wa Rafiki yake na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Hondogo, Kata ya Mandela,Halmashauri ya Chalinze Ndg. Omar Ramadhani. Mh. Ridhiwani amesema Hakika ni Msiba mkubwa sana kwake na wana Chalinze   na Mungu amlaze Mahala pema Peponi. Marehemu Omary Ramadhani, Amin.
LOI1
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Rhidhiwani Kikwete akishiriki kuomba dua  katika msiba  wa marehemu Omary Ramadhani.
LOI2
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Rhidhiwani Kikwete akishiriki kuomba dua  katika msiba  wa marehemu Omary Ramadhani.
LOI3
Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wakishiriki katika mazishi ya Marehemu Omary Ramadhani.
LOI04LOI4
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wakishiriki katika mazishi ya Marehemu Omary Ramadhani.
LOI5
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiweka mchanga katika kaburi wakati wa mazishi ya  Marehemu Omary Ramadhani.

0 maoni:

Chapisha Maoni