Jumamosi, 27 Januari 2018

WAZIRI WA TAMISEMI SELEMAN JAFO AWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KILOSA NA KUIPONGEZA KAMATI YA MAAFA MKOANI MOROGORO

Posted by Esta Malibiche ON JAN 27,2018 IN NEWS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na waathirika wa mafuriko
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa mkoa wa morogoro Dk.Stephen Kebwe wakimtembelea mmoja wa waathirika wa mafuriko ambaye pia ni mlemavu ambaye kwasasa anaishi katika hema.

Baadhi ya madaraja yaliyosombwa na mafuriko wilayani Kilosa.

Wananchi wa Kilosa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu athari za mafuriko Kilosa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akikagua maeneo yaliyoathirika mafuriko.

.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuangalia maafa za mafuriko yaliyo tokea wilayani Kilosa.

     ..................................................................

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo ameipongeza kamati ya maafa ya mkoa morogoro na ya wilaya ya Kilosa kwa juhudi kubwa wanayo ifanya katika zoezi la kuwaokoa wananchi walikumbwa na mafuriko.

Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea wilayani Kilosa leo ili kujionea athari za mafuriko na kuwapa pole waathirika hao. 

Waziri Jafo amewahakikishia waathirika hao wa mafuriko kwamba serikali itajitahidi kufanya mambo ya msingi ili kunusuru maisha ya watu wote.

Amesema serikali itajitahidi kurekebisha miundombinu iliyoathirika ikiwemo barabara, madaraja, shule, Reli, vyanzo vya maji, na huduma mbalimbali za kijamii.  

Katika ukaguzi wake,Jafo amesema kutokana na eneo la tuta la kuzuia maji kubomoka pamoja na mfereji wa kuchepushia maji yaliyozidi ameagiza wataalam wa mradi wa mabadiliko ya tabia nchi wafanye tathmini ili kuona cha kufanya ili kuepusha maafa makubwa kwa siku za usoni kwa maeneo ya mji wa Kilosa na viunga vyake.

Kwasasa wanaendelea kuhamishiwa sehemu ya ukanda wa juu wa Kilosa ambapo serikali imeamua kutenga eneo maalum na kuwapimia viwanja bure ili wananchi wajenge makazi ya kudumu na kuachana na tabia ya kukaa maeneo hatarishi ya mabondeni. 

Aidha serikali kwa kushirikiana na  wadau mbalimbali  inaendelea kuwasaidia mahema, madawa, maji, na chakula ili kukidhi hali ya maisha. 

0 maoni:

Chapisha Maoni