Posted by Esta Malibiche On JAN 24,2018 IN SIASA
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Keri James akizungumza na wanajumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Chama na jumuiya zake katika kikao kilichofanyika Manispaa ya Iringa katika ukumbi wa Hall Faer |
Iringa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Kheri James amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Iringa kuhakikisha zinatenga eneo maalum na rafiki kwa ajili ya vijana wajasiliamali kabla hawajawafukuza katika maeneo yasiyo rasmi wanayofanyia kazi.
Agizo hilo amelitoa jana wakati akizungumza na umoja wa vijana CCM Mkoa wa Iringa,wanachama wa Chama cha Mapinduzi na jumuiya zake,ambapo lisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona vijana wanaondolewa tena kwa kupigwa katika maeneo wanayofanyia kazi zao pasipo kuambiwa wanatakiwa waende wapi,hivyo kila "Halmashauri ihakikishe imetenga eneo kwa ajili ya vijana na kama eneo halijatengwa basi marufuku kuwafukuza nawawaache waendelee na biashara zao.
" Viongozi wa Chama ,Jumuiya na Serikali kwa ujumla hakikisheni mnawatengea vijana eneo lao rasmi la kufanyia kazi kabla hamjawafukuza katika maeneo yasiyo rasmi wanayofanyia kazi zao kwa ajiki yq kujiingizia kipato hivyo kuongeza pato la Taifa na kukuza uchumi."Alisema Kheri na kuongeza kuwa
.Si sahihi na haikubaliki kumwambia kijana atoke katika eneo analofanyia biashara kabla haujamtengea eneo rafiki haitakubalika.Kama mnataka kuwatoa basi hakikisheni mmewapa eneo lao la kufanyia kazi zao kinyume na hapo ni matumizi mabaya ya madaraka."Alisema Kheri"
Aidha aliwataka viongozi wa Uvccm ngazi zote kutenga muda maalum kwa ajili yakupokea maoni kutoka kwa vijana na wanachama ili waweze kuyatatua kwa wakati.
"Nendeni mkawafikie wanachama na kupokea maoni yao na siyo kukaa ofisini tu, lazima tujue kuwa Uvccm ni sauti inayosikikika kwasababu kuna vijana wana mawazo na maoni juu ya Serikali yao lakini hawana pa kusemea.Wafikieni,bodaboda,vijana wajasiliamali,Mama nitilie,vijana wa Vijiweni na wengineo"" Alisiaitiza Kheri
Hata hivyo aliwasihi viongozi wa Uvccm katika ngazi zote kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi ikiwa nipamoja na kutambua mipaka yao ya kufanyia kazi na kuheshimiana iili kuepuka migogoro isiyo ya lazima na inayoweza kuhepukika.
Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Mgala alisema hakuna kiongozi ndani ya Chama na na Serikali kaa asiyepitia na kupikwa na Uvccm,hivyo ni jukumu la Vijana kuienzi kwa vitendo na si kwa mamneo tu.
"Uvccm ni tanuru la kuoka viongozi, mbalimbali ndani ya Chama na Serikali yake ambalo limewekewa namna ya kuongoza ukiwa kiongozi utokana na mafundisho tunayoyapata Uvccm .
Nae Mnec wa Mkoa wa Iringa Salim Asas akizungumza aliwataka Vijana kuchangamkia fursa zinazotokana na Chama cha Mapinduzi CCM.
"Fursa za Vijana zipo ndani ya CCM sababu ndiyo inayotawala na ndiyo yenye Serikali.Hakuna kijana atakaepata fursa nje ya CCM ,hivyo tuache ushabiki usio na tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla""
Alisema Asasas na kuongeza kuwa
"Tuwapuuze watu wanaotugawa vijana nawatanzania kwa ujumla,tusiwashabikie wale wote wasiopenda maendeleo ya Nchi yetu ambao kutwa kuchwa wanaitukana Serikali na viongozi wa Chama,watu kama hawa ni wa kupuuzwa"" Alisema Asas
Ninawaomba tumuombee Mh.Rais wetu kipenzi cha watanzania,Dakta John Magufuli,tumuunge mkono kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutetea mali za watanzania ili tuaweze kunufaika nazo.
Kenani Kihongosi ni Mwenyekiti wa Jumuiyabya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,akizungumza alisema,Vijana ni chachu ya Chama cha Mapinduzi,hivyo wanatakiwa kuisaidia CCM nanSerikali yake ili iendelee kutawala.
"Tuisemee vizuri Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi kwa yote yanayofanywa, tuwe mstari wa mbele kuyatangaza kwa wananchi ili wajue nini kinatekelezwa na Irani ya chama cha Mapinduzi.
Aidha alisisitiza wananchi wamuunge mkono Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa,Rais Dakta John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kwa maslai mapana ya Taifa.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Mgala akizungumza.
Kada wa Chama cha Mapinduzi CCMambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Asia Abdalah akizungumza.
Mioni mwa wqnachama wapya wqliorejesha kadi za Chadema na kujiunga na Chama cha Mmapinduzi CCM.
Mwanachama Mpya miongoni mwa 448 waliojiunga na Chama cha MapinduI CCM akipokea kadi tayari kwa kiapo.
Wanachama wapya 448 waliojiunga na Chama cha Mapinduzi CCM,wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi na wengine kurejesha kadi za Chadema. |
Mwenyekiti wa uvccm Taifa alikutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza na kufanya mazungumzo Ofisini kwake,ambapo Mkuu wa Mkoa aliipongeza Jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM kwakuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais John Magufuli kwa kuyasemea mazuri yote yanayofanywa na Serikali.
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Kheri Jemes alitembelea na kukagua chuo cha Mafunzo ya makada Ihemi n kuzungumza na watumishi wa chuo hicho.
Katika mazungumzo yao alisema Chama cha Mapinduzi kitaendelea kutimiza ndoto za wazee ambao ni Asisi wa Chama kwa kuifanya Ihemi kuwa kimbilio la vijana kimafunzo, Taaluma na Uchumi wa Jumuiya.
Mwenyekiti waa Uvccm Taifa Kheri Jemes alitembelea na kukagua chuo cha Mafunzo ya makada Ihemi kuzungumza na watumishi wa chuo hicho.
Katika mazungumzo yao alisema Chama cha Mapinduzi kitaendelea kutimiza ndoto za wazee wa Chama kwa kuifanya Ihemi kuwa kimbilio la vijana kimafunzo, Taaluma na Uchumimna wa Jumuiya.
0 maoni:
Chapisha Maoni