Posted by Esta Malibiche on FEB10,2017 IN MICHEZO
Shirikisho la soka Ulimwenguni
(FIFA) hapo jana limetoa orodha mpya ya ubora wa viwango vya soka
Duniani kwa nchi Wanachama , na Vinara wake bado ni Argentina wakifuatia
Brazil na kwa Afrika ni Misri ndio wapo juu kabisa huku Tanzania
ikishuka Nafasi 2 na kukamata Namba 158.
5 Bora kwenye orodha hiyo zimebaki
zile zile bila mabadiliko na nazo ni Argentina (1), Brazil (2), Germany
(3), Chile (4) na Belgium (5).
Kwa Afrika, Nchi ambayo iko juu
kabisa ni Misri, waliotolewa Fainali ya AFCON 2017, ambao sasa wapo
Nafasi ya 23 baada kupanda Nafasi 12 wakifuata Senegal walio Nafasi ya
31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao ni Cameroon, wapo Nafasi ya 33
baada kupaa Nafasi 29.
Orodha hiyo ni;
- Argentina
- Brazil
- Germany
- Chile
- Belgium
- France
- Colombia
- Portugal
- Uruguay
- Spain
- Switzerland
- Wales
- England
- Poland
- Italy
- Croatia
- Mexico
- Peru
- Costa Rica
- Iceland
Kwa upande wa Afrika Uganda bado
wanaendelea kuongoza kwa Afrika Mashiriki wakiwa nafasi ya 17 kwa Afrika
na 75 duniani wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 20 Afrika na 87
duniani wakati Rwanda wako nafasi ya 27 Afrika na 100 duniani na Burundi
nafasi ya 40 Afrika na 138 duniani
Kwa upande wa Afrika Misri
wamekuwa vinara kwa kukwea kwa nafasi 12 na kutua kileleni wakiwa nafasi
ya 23, wakifuatiwa na Senegal walioko nafasi ya 31 huku mabingwa wa
michuano ya Mataifa ya Afrika Cameroon nao wakikwea kwa nafasi 29 mpaka
nafasi ya 33 duniani.
0 maoni:
Chapisha Maoni