Posted by Esta Malibiche on FEB 10,2017 IN NEWS
Mkuu wa Iringa Amina Masenza akisalimiana na walimu wa shule ya sekondari Lundamatwe Kilolo |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikagua vyumba vya madarasa |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Lundamatwe wilaya ya kilolo |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikagua madaftari ya wanafunzi shule ya sekondari Lundamatwe wilaya ya kilolo wakati wa ziara yake |
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah kushoto akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa kikao cha majumuisho wilayani Kilolo |
Na matukiodaima blog ,Kilolo
SERIKALI ya Mkoa wa Iringa imeagiza wazazi walioshindwa kupeleka Watoto waliofaulu kujiunga na sekondari wasakwe .
Agizo hilo imetolewa leo na mkuu wa
Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa vyumba
vya madarasa kwenye Shule za sekondari wilaya ya Kilolo.
Alisema kuwa ni wajibu wa watendaji wa
vijiji na kata kushirikiana na Walimu wakuu wa Shule pamoja na waratibu
Elimu kata kujua idadi ya Watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha
kwanza kuona wameripoti Shule.
” Nawaagiza watendaji wote kufanya msako wa watoto walioshinda kujiunga na elimu ya sekondari”
Alisema mbali ya Watoto hao kusakwa
pia lazima wazazi wabanwe kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wao wa
kupeleka Watoto Shule
Mkuu alisema lengo la serikali ya
awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ni kuona kila mtoto
anakwenda Shule na ndio sababu ya kufuta ada.
Hivyo alisema kwa mazazi atakayeshindwa kusomesha mtoto anapaswa kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.
Alisema mfano katika Shule ya
sekondari Lundamatwe kati ya Watoto waliopaswa kujiunga na sekondari
hadi sasa ni Watoto wanne ndio walichelewa kujiunga ila baada ya wazazi
kubanwa Watoto.
Wawili wameripoti na Watoto wawili
wanasakwa na kwa wilaya asilimia 17.89 ya Watoto waliochaguliwa kujiunga
sekondari hawajaripoti.
“Naagiza hawa Watoto wawili waliokaa
nyumbani watafutwe na waletwe Shule kama suala ni umbali wa Shule basi
waletwe kuishi Hosteli “
Kuhusu maabara mkuu huyo alisema bado
kuna changamoto kubwa ya maabara kutokana na wilaya hiyo kugeuza vyumba
vya madarasa kuwa maabara hivyo kupelekea upungufu vya vyumba vya
madarasa pamoja na maabara zilizo nyingi kuwa chini ya kiwango.
Masenza alimwagiza mkuu wa wilaya ya
Kilolo Asia Abdalah na uongozi wa halmashauri ya kilolo kufanya
jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara borabora.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah
alisema kuwa kasi ya kuwabana wazazi wasiopeleka Shule Watoto
inaendelea na wametoa muda hadi machi wazazi wote kupeleka Watoto wao
Shule.
Kwa mujibu wa Afisa Elimu Kilolo
Stephen Mrosso jumla ya wanafunzi 3734 ndio walichaguliwa kujiunga na
sekondari kati yao wavulana 1658 na wasichana 2076 wanafunzi walioripoti
ni 2987 wavulana 1287 na wasichana1693.
Wakati wanafunzi ambao hawajaripoti ni
747 wasichana 383 na wavulana 364 kuwa taarifa zilizopo wanafunzi 82
wakiwemo wavulana 36 na wasichana 46 wamejiunga na Shule nyingine nje ya
wilaya ya Kilolo na kufanya jumla ya wanafunzi waliopo Shule kufikia
3069 sawa na asilimia 82.19 hivyo bado asilimia 17.89 kuripoti shule
Mwisho
0 maoni:
Chapisha Maoni