Jumatatu, 6 Februari 2017

CAMEROON BINGWA AFCON 2017,YALIPA KISASI DHIDI YA MISRI

posted by Esta Malibiche on FEB 6,2017 IN MICHEZO

 Cameroons-Vincent-Aboubakar-celebrates-scoring-their-second-goal-with-teammates-and-staff
Timu ya Taifa ya Cameroon imelipa kisasi cha Fainali ya 2008 ilipofungwa na Misri hatimaye nayo Imetwaa taji la Michuano ya Afrika ‘AFCON’ 2017 nchini Gabon baada ya kuwatandika Mafarao jumla ya magoli 2-1 na kubeba Ubingwa huo.
Leo ndiyo mwisho wa michuano ya Afcon na Cameroon ambayo haikupewa nafasi sana imekwenda nyumbani na kombe hilo.
 
Misri ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mohamed Elneny katika dakika ya 22, bao hilo likadumu hadi mapumziko.

Cameroon walisawazisha bao lao katika dakika ya 59 mfungaji akiwa Nicholas Nkoulou kwa kichwa na Vicent Aboubakar akafunga bao safi katika dakika ya 88 na kukamilisha ndoto ya Cameroon kubeba ubingwa huo.

0 maoni:

Chapisha Maoni