Posted by Esta Malibiche on FEB 14,2017 IN NEWS
Msimamizi
wa mradi huo toka Kampuni ya Serengeti Ltd Bw.MehrdadTalik (katikati)
akisitiza Jambo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Maji
Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Romanus
03.Mwang'ingo (kushoto) wakati wa ziara ya waandishi wa habari
kutembelea mradi wa uchimbaji Visima virefu katika eneo la Kimbiji kulia
ni mshauri wa mradi huo Bw. Roland Chombo.
Serikali
kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)
inatekeleza mradi wenye thamani ya bilioni 18 unaolenga kuondoa
changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa ufundi na uendeshaji wa Mamlaka
hiyo Bw. Romanus Mwangingo wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika
eneo la Kimbiji ambako ndipo mradi huo unapotekelezwa .
“Mkandarasi
anaendelea na kazi na ameleta mabomba yote na amechimba visima 15 na
vitazalisha maji yatakayotumika katika Jiji la Dar es salaam na mradi
unatarajiwa kukamilika machi 2017” Alisisistiza Mwangingo.
Aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 85 na
utakapokamilika maeneo ya Kigamboni,Temeke,Ilala na Jiji la Dar es
salaam kwa ujumla yatanufaika kwa kupata huduma ya maji.
Kwa
upande wa miradi mingine kama ule wa ujenzi wa Bomba kutoka Ruvu juu
hadi kimara Mwangingo amesema ulikamilika mwezi oktoba 2016 na
uzalishaji wa majaribio unaendelea.
Mradi
huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 59 ni moja ya mikakati
ya Serikali katika kuhakikisha kuwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam
wanapata huduma ya maji safi na salama. na kuondokana na changamoto
hiyo. .
Aidha mradi huo utawezesha kiwango cha maji kufikia lita milioni 196 kwa
siku kutoka lita milioni 82 za awali.
Kwa
upande wake Bw.Salum Hamis mkazi wa mbagala amepongeza miradi ya maji
inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi kwa kuwa imekuwa
chachu ya maendeleo katika maeneo yao.
Aliongeza kuwa miradi hiyo imechochea kupunguza tatizo la maji na
imewawezesha wananchi kutumia muda mwingi katika shughuli za kiuchumi na
hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.
Katika
kukabilina na tatizo la miundombinu ya maji taka katika Jiji la Dar es
salaam mamlaka hiyo iko katika mchakato wa kuanza ujenzi wa mtambo
mkubwa wa kuchuja maji taka katika eneo la Jangwani na kuboresha mfumo
wa maji taka katikati ya Jiji.
Mradi
mwingine ni ule wa upanuzi wa ruvu chini ambao umekamilika kwa asilimia
mia moja na utawezesha upatikanaji wa maji kufikia lita milioni 270 kwa
siku kutoka milioni 180 kabla ya mradi huo haujatekelezwa.
Majukumu
ya DAWASA ni kumiliki miundombinu ya maji safi na maji taka kwa niaba
ya Serikali, kusimamia utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka Dar es
salaam, kugharimia,kupanga mipango na kusimamia upanuzi wa huduma na
kuishauri Serikali kuhusu masuala ya huduma ya maji safi na maji taka
Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es
Salaam (DAWASA), Mhandisi Romanus Mwang'ingo akiwaeleza waandishi wa
habari kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa changamoto ya
upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam inapatiwa ufumbuzi wa
kudumu mara baada ya kukamilika kwa miradi ya Ruvu Juu na Chini pamoja
na ule wa uchimbaji wa Visima Virefu katika eneo la Kimbiji
vitakavyozalisha maji yatakayotumika katika Jiji la Dar es salaam
Meneja
Uhusiano wa DAWASA Bi Neli Msuya akieleza kwa waandishi wa habari faida
za miradi inayoibuliwa na Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wananchi
katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es
salaam.
Maji
yakitoka kwenye moja ya Kisima Kirefu kilichochimbwa katika eneo la
Kimbiji unakotekelezwa mradi mkubwa wa unaolenga kutatua changamoto ya
maji katika Jiji la Dar es salaam.
Mtambo unaotumika kuchoronga Visima Virefu ukiwa katika eneo la Kimbiji unapotekelezwa mradi mkubwa wa uchimbaji visima virefu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mladi,Salum Selenge akionesha tanki linalotumika kuhifadhi
maji katika miradi iliyobuniwa na DAWASA katika eneo la mbagala na
kuendeshwa na wananchi wenyewe ikiwa ni mkakati wa Mamlaka hiyo kuibua
miradi ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar
es salaam.
Sehemu ya Kisima kama inavyoonekana katika
0 maoni:
Chapisha Maoni