Posted by Esta Malibiche on FEB 16,2017 IN NEWS
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leonard Chamuriho
(kushoto) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bi.
Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la
Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini
Mwanza.
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leornard Chamurho
(kushoto), akifurahia maelezo yanayotolewa na Meneja wa Kiwanja cha
Ndege cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja
vya ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la
Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria
linalofanyika jijini Mwanza.
Mhandisi Diana Munubi (wa kwanza
kulia) akitoa maelezo yaliyomfurahisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dtk. Leonard Chamurho (wa
kwanza kushoto), akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,
Prof. Faustine Kamuzora, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo na Afisa Usafirishaji Mkuu wa
Uchukuzi, Alphonce Mwingira katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la
Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria
linalofanyika jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) kutoka taasisi za TAA, TCAA,
TMA na DMI wanaoshiriki kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la
Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria,
linalofanyika Mwanza, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu
Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamurho, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Prof.
Faustine Kamuzora, na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
Dkt. Frank Mgeta wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure (kulia), akipata maelezo mbalimbali
yanayohusu mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya washiriki wa
Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa
Victoria, jijini Mwanza.
Raia wa Kenya, John Osodo
(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi (kulia)
alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
kwenye maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi
Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika Jijini Mwanza.
0 maoni:
Chapisha Maoni