Posted by Esta Malibiche on FEB 16,2017 IN NEWS
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) leo Jumatano Februari 15,2017 ameanza ziara ya kukagua
miradi ya maendeleo na kuangalia miundo mbinu iliyopo katika jimbo hilo.
Siku ya kwanza ya ziara ya mbunge huyo ilikuwa katika kata ya Kolandoto,Ibadakuli,Shinyanga Mjini,Kambarage na Ngokolo.
Mheshimiwa
Masele alikuwa ameambatana na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga
Mjini Rajabu Makuburi pamoja na wataalam kutoka idara mbalimbali katika
manispaa ya Shinyanga.
Mheshimiwa
Masele ametembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja lililopo katika
kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga ambalo
lipo kati mto mkubwa maarufu kwa jina la ‘Mto Simba’.
Mbunge
huyo pia amejionea jinsi barabara ya kutoka barabara kuu ya Shinyanga –
Mwanza kwenda hospitali ya Kolandoto ilivyokatika na kusikiliza kero za
wananchi katika kata ya Kolandoto.
Ziara ya
Mbunge Masele pia ilifika katika masoko makubwa yaliyopo katika jimbo
hilo ikiwemo soko la Kambarage lililopo kata ya Kambarage,Nguzo Nane
lililopo kata ya Shinyanga mjini,soko kuu la mkoa wa Shinyanga na soko
la Mitumba maarufu ‘Ngokolo Mitumbani’ lililopo kata ya Ngokolo katika
manispaa ya Shinyanga.
Mwandishi
mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo katika ziara hiyo
ametuletea picha 44 za matukio yaliyojiri kuanzia mwanzo hadi mwisho wa
ziara ya Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele.
Hapa ni
katika Barabara ya Kolandoto- Wami ambayo inatoka katika barabara kuu ya
Shinyanga- Mwanza-Kushoto ni Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya
Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akimuonesha mbunge wa jimbo la
Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele (wa pili kushoto) jinsi
barabara hiyo ilivyomong’onyoka hali inayotishia kukatika kwa barabara
hiyo inayoelekea katika hospitali ya Kolandoto.
Mhandisi
wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akiendelea
kutoa maelezo ingawa hata hivyo mbunge Masele aliahidi
kutengenezwa/kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango kwa fedha za mfuko
wa jimbo la Shinyanga mjini wakati wanafanya utarabu wa kujenga barabara
hiyo katika kiwango cha lami.
Hapa ni
katika Ofisi ya CCM Kata ya Kolandoto-Aliyesimama ni Katibu Mwenezi wa
CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akizungumza wakati
akimkaribisha mheshimiwa Masele aweze kuzungumza na baadhi ya wananchi
wa kata hiyo huku akibainisha kuwa ziara hiyo inalenga kutekeleza ilani
ya uchaguzi ya CCM.
Diwani wa
Kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya ambaye pia ni Naibu Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Shinyanga akielezea changamoto ya gharama kubwa za
matibabu katika hospitali ya Kolandoto hali inayosababisha wananchi wa
eneo hilo wakose huduma ya afya kama inavyotakiwa matokeo yake
kulazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma hiyo katika
kituo cha Afya Kambarage au Zahanati ya Galamba.
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi wa kata ya Kolandoto ambapo
alisema ziara hiyo siyo ya siasa bali ni kiutendaji.
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) alieleza kukerwa na changamoto ya gharama kubwa ya
matibabu katika hospitali ya Kolandoto na kuahidi kuzungumza na mamlaka
zinazohusika ili kumaliza tatizo hilo.Mheshimiwa Masele pia alisema
serikali/Chama Cha Mapinduzi kinafanya jitihada zote ili kuhakikisha
kuwa wananchi wa kata ya Kolandoto wanapata huduma ya maji safi na
salama.
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akimwelezea Mheshimiwa Masele changamoto zilizopo katika kata hiyo
Mkazi wa Kolandoto Kadesha Noniyaza akielezea kero ya maji katika kijiji cha Wami na Mwanubi
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi katika Senta ya kijiji cha
Galamba kilichopo katika kata ya Kolandoto baada ya kumuomba asimame
wamwelezee changamoto zinazowakabili ambazo ni maji na uhitaji wa daraja
katika mto Simba
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na
wananchi hao na kuwaeleza namna serikali inavyojitahidi kuhakikisha kuwa
kero zao zinamalizika
Hapa ni
katika Mto Simba ambapo mradi wa Ujenzi wa Daraja lililopo katika kijiji
cha Galamba kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga unaendelea.Pichani
ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM)
akiangalia upande wa pili wa daraja linalojengwa na Mkandarasi M/S
Pasons Co.Ltd tangu mwezi Juni mwaka 2016 na unatarajia kukamilika mwezi
Machi mwaka 2017.
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia
daraja hilo ambalo mpaka kukamilika kwake jumla ya shilingi milioni
429.8 zinatarajiwa kutumika.
Mmoja wa
wataalam katika ujenzi huo akimwelezea mbunge wa jimbo la Shinyanga
Mjini mheshimiwa Stephen Masele namna ujenzi huo unavyoendelea.
Daraja hilo lina urefu wa mita 26 na upana wa mita 8
Ujenzi wa daraja ukiendelea
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishindilia zege kwa kutumia mashine kwenye daraja hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza kwenye
daraja la Galamba ambapo alisema ujenzi huo wa daraja ambalo litaboresha
mawasiliano katika kata ya Kolandoto na manispaa ya Shinyanga kwa
ujumla ni miongoni mwa ahadi ambazo aliahidi wakati wa kampeni za
uchaguzi mwaka 2015
Diwani wa
kata ya Kolandoto Agnes Machiya (CCM) akizungumza ambapo alisema mradi
huo unatekelezwa kupitia mfuko wa barabara ‘Road Fund’ huku akiongeza
kuwa daraja hilo litaunganisha wilaya ya Shinyanga,Wilaya ya Kishapu na
Meatu na kwamba kabla ya ujenzi huo eneo hilo lilikuwa kero hasa wakati
wa masika
Mkandarasi
George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd akielezea mradi huo wa daraja
ambapo alisema mpaka sasa ameshakamilisha ujenzi wa vitako vyote vya
daraja na ujenzi wa kuta/nguzo zote za daraja na kwamba anaendelea
kutengeneza kindanda cha daraja ya upande mmoja na kwamba ujenzi
umekamilika kwa asilimia 75.
Muonekano wa daraja hilo
Ujenzi unaendelea
Muonekano wa daraja na eneo ambapo mto Simba unapita
Mheshimiwa Masele akiteta jambo na Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd
Hapa ni
katika Shule ya Msingi Bugweto iliyopo kata ya Ibadakuli katika manispaa
ya Shinyanga-Wanafunzi na walimu wakimpokea mbunge wa jimbo la
Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akimtambulisha
Diwani wa viti maalum (CCM) kata ya Ibadakuli mheshimiwa Zuhura Waziri
(katikati) na diwani wa kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya (CCM)
ambaye pia naibu meya wa manispaa ya Shinyanga
Mheshimiwa
Masele akizungumza katika shule ya msingi Bugweto na kuwataarifu
wanafunzi na walimu wa shule hiyo kuwa ametoa mifuko 100 ya saraji kwa
ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo ambayo yamechakaa na hayana
sakafu sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa katika picha
ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Bugweto
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya darasa la saba katika shule ya msingi Bugweto
Darasa likiwa lina kokoto na vumbi sakafuni
Hapa ni
katika Soko la Kambarage kata ya Kambarage katika Manispaa ya
Shinyanga.Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele
akiwasili katika soko hilo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyabiashara
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akisalimiana na
mfanyabiashara katika soko la Kambarage katika manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na
wafanyabiashara katika soko la Kambarage na kuwaeleza kuwa serikali ina
mpango wa kujenga upya soko hilo hivyo kuwaomba wafanyabiashara wakae na
viongozi wao na manispaa ya Shinyanga waangalie eneo ambalo litatumika
wakati wakipisha ujenzi wa soko hilo pia kuangalia mazingira mazuri ya
wafanyabishara hao kurudi na kuendelea na biashara katika soko hilo
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiteta jambo na
katibu wa soko la Kambarage Daudi Kitila( wa kwanza kulia)
Hapa ni
katika eneo la Stendi Mpya ya Mabasi Mjini Shinyanga ambapo ujenzi wa
choo cha stendi hiyo unaendelea.Katikati ni Mhandisi wa Barabara wa
Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akielezea ujenzi wa mfumo
wa majitaka unaoendelea katika eneo hilo
Hapa ni katika soko la Nguzo Nane kata ya Shinyanga Mjini-Mheshimiwa Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akisikiliza na
kujibu kero za wafanyabishara katika soko hilo.Kero kubwa iliyotolewa ni
ushuru mkubwa kwa mazao ambapo Masele aliahidi kukutana na uongozi wa
manispaa ya Shinyanga kufuatilia kero hiyo na namna ya kuitatua
Ndani ya
Soko Kuu la Mkoa wa Shinyanga.Mheshimiwa Masele akizungumza na
wafanyabiashara katika soko hilo,kero kubwa ikiwa ni soko hilo kukosa
wateja kutokana wafanyabiashara na wateja kukimbilia katika soko la
Nguzo Nane na Kambarage
Hapa ni
Ngokolo Mitumbani,kwenye soko la Mitumba lililopo kata ya Ngokolo katika
manispaa ya Shinyanga.Mheshimiwa Mbunge akishangaa namna mabanda
yalivyo wazi kutokana na wafanyabiashara kukimbia soko hilo na kufanyia
biashara zao katika maeneo mengine mjini Shinyanga
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na
wafanyabiashara wa nguo za mitumba katika soko la Mitumba,maarufu
Ngokolo Mitumbani katika kata ya Ngokolo.
Mfanyabiashara
wa Mitumba akielezea jinsi soko hilo lilivyokosa wafanyabiashara
kutokana serikali kuruhusu masoko kila mahali mjini Shinyanga
Vibanda vikiwa havina nguo
Mbunge wa
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akijadiliana na
wafanyabiashara hao namna ya kurudisha wafanyabiashara waliokimbia
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
0 maoni:
Chapisha Maoni