Posted by Esta Malibiche on FEB 13,2017
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki
ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi
rasmi wa tawi la kisasa la benki hiyo katika jengo la Shirika la Nyumba (NHC),
mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na kulia ni
Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Dk. Suleman Mohamed.
Mkuu wa Mauzo wa Benki ya
Barclays Tanzania, (kushoto), akieleza kuhusu huduma mbalimbali za kibenki
zitolewazo katika tawi jipya Barclays la mjini Morogoro katika sherehe za
uzinduzi wa tawi hilo juzi. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Abdi
Mohamed, mjumbe wa bodi, Dk. Suleman Mohamed na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya
Benki ya Barclays, Simon Mponji .
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki
ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa
habari katika hafla ya uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo mjini Morogoro. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Barclays, Abdi Mohamed na Mjumbe wa Bodi
ya benki hiyo, Dk. Suleman Mohamed.
Meneja Masoko wa Barclays, Joe
Bendera (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya uzunduzi
wa tawi hilo.
Wafanyakazi wa Benki ya Barclays
Tawi la Morogoro wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya viongozi wa
benki hiyo mara baada ya hafla ya uzinduzi wa tawi hilo.
Moja ya burudani zilizokuwepo
wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi la Benki ya Barclays mjini Morogoro juzi.
0 maoni:
Chapisha Maoni