Posted by Esta Malibiche on FEB 13,2017 IN NEWS
Afisa
Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimpima
mapigo ya moyo Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Dodoma Mariam
aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya
moyo. JKCI ilishiriki katika kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na
kupima afya bila malipo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee
na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri jumla ya wagonjwa 408
walihudumiwa katika banda hilo.
Mtaalamu
wa Afya na Mazoezi ya viungo kutoka Chama Cha Wafanya Mazoezi Tanzania
Waziri Ndonde akiwaelekeza wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima
magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
umuhimu wa kufanya mazoezi na aina ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya.
Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua
kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa
muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Mtaalamu
wa Dawa na Tiba kutoka Hospitali ya SANITAS Dk. Sajjad Fazel
akiwafundisha wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya
moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina ya
vyakula bora wanavyotakiwa kula ili waepukane na magonjwa
yasiyoambukiza. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni
ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila
malipo kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Mratibu
wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watu wazima na magonjwa ya
saratani kutoka Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Sara
Maongezi akiwafundisha wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima
magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
aina za saratani na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara. Hivi karibuni
Wizara hiyo ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima
afya bure kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Twaha
Dofa (aliyeshika karatasi) akitoka kupima magonjwa ya moyo katika banda
la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa
siku mbili iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,
Wazee na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Pedro Pallangyo akimsikiliza mtoto Oliva Mushi aliyefika katika banda la
Taasisi hiyo kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya Moyo. Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto ilizindua kampeni ya
kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo Mkoani Dodoma
ambapo wananchi wa mkoa huo walipimwa afya zao bila malipo kwa muda wa
siku mbili zoezi lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri.
Utamaduni wa Mtanzania ni Sehemu ya Kivutio cha Utalii: Waziri Nape.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza
wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na
Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli
mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na
kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla
akizungumza wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya
Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa
na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza
na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Balozi
wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng (wa pili
kutoka kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) wakati wa kilele cha Wiki
ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla, Mkurugenzi wa Kituo cha
Utamaduni cha Iran Ali Bagheri na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akicheza Bao
na Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Jadi Tanzania Bw. Mohamed
Kazingumbe (kulia) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni
baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo
yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya
kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Baadhi
ya Wasanii kutoka Iran wakitumbuiza muziki wa Ala wakati wa kilele cha
Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini
Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa
Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na
Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia
moja ya vitabu vyenye maneno ya Kishiraz wakati wa kilele cha Maonyesho
ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es
Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa
Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na
Filamu,Mila na desturi zake”. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Utamaduni Bibi. Lilian Beleko, Balozi wa Iran nchini Mossa
Farharng na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza
maelezo kuhusu michoro ya Kiutamaduni ya Iran wakati wa kilele cha
Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini
Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa
Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na
Filamu,Mila na desturi zake”.
:
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye
akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bw. Benson Mkenda alipotembelea meza ya Bodi hiyo wakati wa
kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania
jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya
“Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza
Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia
jambo mara baada ya kupata maelezo ya namna ya kufanya marekebisho ya
Vitabu kutoka kwa Ali Navidogooe Shiraz wakati wa kilele cha Maonyesho
ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es
Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa
Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na
Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akipiga Gitaa
lililotengenezwa na Msaanii wa Uchoraji na Uchongaji Bw. Washington
Steven Masanja (kushoto) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya
Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es
Salaam.Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa
Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na
Filamu,Mila na desturi zake”. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mtendaji wa
Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Wasanii
wa Mashairi Bw. Issa Amiri Kilimo aka. Kijoka Kidogo na Mwajuma Seleman
Yombe wakiimba shairi kwa njia ya majibizano ikiwa ni kujibu shairi la
Siri la mtunzi Haji Myaka bin Haji la mwaka 1405 jana jijini Dar es
Salaam wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya
Shiraz na Tanzania.
Balozi
wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng akimkabidhi
zawadi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye
wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika
ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia
jambo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa
Farharng wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika
katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiwa katika
picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania
Mossa Farharng na baadhi ya viongozi kutoka taasisi za Serikali na
ubalozi wa Iran wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz
iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam
jana.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
…………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Serikali
chini ya Wizara ya Hbari Utamaduni Sanaa na Michezo inaendelea na
juhudi za kuhakikisha kuwa Utamaduni wa Mtanzania unakuwa sehemu ya
muhimu ya kivutio cha Utalii ili kutengeneza ajira na kuingizia Serikali
mapato.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Nnauye alipokuwa anafungwa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi
yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa madhimisho
haya yanaimarisha undugu wa damu wa kiuchumi na kiutamaduni ulioachwa na
wahenga.
“Maadhimisho
ya wiki ya Utamaduni wa Shirazi ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwa
kwa wairani namna ya kukuza ,kulinda na kuendeleza
Utamaduni,Sanaa,Filamu,Mila na Desturi zetu”Alisema Waziri Nape.
Aidha
ameongeza kuwa Wizara yake itaweza kufanikisha shughuli za Utamaduni
na kuziendeleza kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya ya nchi
kama ilivyofanyika katika maadhimisho ya mwaka huu kwani yanatangaza
vikundi vya Sanaa na Wasanii.
Kwa
upande wa wake Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Irani hapa nchini
Bw.Ally Baghari amesema kuwa ushirikiano wa Kiutamaduni baina ya
Tanzania na Irani umeongeza mafanikio ya kiuchumi na kijamii katika nchi
hizo hasa kupitia ubadilishanaji wa Utamaduni tangu enzi za ukoloni.
“Tumejifunza
utamaduni wa kitanzania kupitia maadhimisho haya na tunaamini
watanzania pia wamejifunza utamaduni wa Irani ambao umesaidia kuimarisha
ushirikiano wetu”Alisema Bw Baghari.
Maadhimisho
hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo
muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi
zake”.
0 maoni:
Chapisha Maoni