Posted by Esta Malibiche on FEB 10,2017 IN NEWS
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAD,
Bw. Francis Assenga (Katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Hazina na
Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru (Watatu kushoto) wakiwa na wenyeji
wao Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga (wa pili
toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Kilimo ya Morocco (Credit Agricole) Bw. Jamal Eddine Wl
Jamali (Katikati). Wengine ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha
wa TADB Bw. Albert Ngusaru na Wakurugenzi wawili wa Benki ya Credit
Agricole Bi. Dkhil Mariem (Kushoto) na Bi Leila Akhmisse (Kulia).
Ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB) ukipatiwa maelezo juu ya miradi ya kilimo
inavyoendeshwa nchini Morocco wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB
Bw. Francis Assenga (Mwenye Kaunda Suti) na Bw. Albert Ngusaru
Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha (Mwanye Daftari) walipotembelea
Morocco wiki hii kuanza utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano kati ya
TADB na GCAM.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bw. Francis Assenga (Katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Credit Agricole na Tamwil El
Fellah wakati walipokagua miradi mbalimbali ya kilimo na ufugaji katika
vijiji vya mji wa Khemisset nchini Morocco jana. Kulia kabisa ni Bw.
Albert Ngusaru ambaye ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa
TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga (kushoto)
akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki
ya Kilimo ya Morocco (Credit Agricole) Bw. Jamal Eddine W. Jamali
(Katikati). Kulia ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB
Bw. Albert Ngusaru.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kushoto)
akiwa na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB Bw. Albert
Ngusaru (Kulia) walipotembelea Benki ya Kilimo ya Morocco (Credit
Agricole).
…………….
Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) imeanza kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Ushirikiano
uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Morocco wakati wa Ziara ya
Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI alipotembelea Tanzania kwa mwaliko
wa Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli mnamo mwezi Oktoba 2016.
Katika kutekeleza makubaliano
hayo, ujumbe wa TADB ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Francis
Assenga na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru
upo nchini Morocco, pamoja na mambo mengine kuainisha maeneo ambayo
Benki hiyo itashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco
(GCAM) na kuwekeana mikakati ya utekelezaji.
Kwa mujibu wa Bw. Assenga, pamoja
na kupanga mikakati hiyo, ujumbe huo ulipata fursa ya kukagua miradi
kadhaa ya kilimo na ufugaji ambayo Tanzania inaweza kuianzisha kwa
mafanikio.
TADB imeanzishwa kwa malengo makuu
ya Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni
endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo
kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
0 maoni:
Chapisha Maoni