Posted by Esta Malibiche on FEB 6,2017 IN NEWS
Kiasi cha Shlilingi Trilioni 48
kinahitajika kutoka Sekta Binafsi ili kufanikisha ujenzi wa miradi
mikubwa ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa
unaotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango, amesema hayo mjini Dodoma wakati akifunga semina ya siku moja
iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPS iliyohusu
zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta
Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private
Equity Project)
“Imekadiriwa kuwa mahitaji ya fedha
ya mpango huo ni takriban shilingi Trilioni 107, kati ya hizo shilingi
Trilioni 59, sawa na asilimia 55, zitatokana na mapato ya Serikali na
shiilingi Trilioni 48, sawa na asilimia 45 zitatokana na vyanzo vya
Sekta Binafsi,” alisema Mpango.
Amesisitiza umuhimu wa Sekta Binafsi
kuwekeza zaidi kwenye kilimo na viwanda vitakavyosaidia kuongeza thamani
ya mazao ya wakulima ili waweze kunufaika kiuchumi na kuendeleza nchi
kwa ujumla.
Dkt. Mpango, ameahidi kuwa Serikali iko
tayari kuhakikisha kuwa vitendea kazi muhimu vya utekelezaji wa mradi
huo vinapatikana ili kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo ya ubia
ukiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es salaam
kwenda Chalinze.
Benny Mwaipaja, Dodoma
0 maoni:
Chapisha Maoni