Posted by Esta Malibiche ob FEB 27,2017 IN NEWS
Mbunge
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji
kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe
manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati
wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mbunge
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye
pia ndiye aliyechimba kisima hicho.
Mbunge
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa
Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Mbunge
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akiangalia maji waliyokuwa wakitumia wananchi wa mtaa huo
Maji yaliyokuwa yakitumiwa awali na wananchiwa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima
Wananchi
wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa wamemshukuru mbunge wa viti
maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima
cha maji safi na salama.
Wakizungumza
na blog hii wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na
tatu (53) hawajawahi pata maji masafi na salama.
“Angalia
maji haya machafu ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa
anatusaidia tu kutuepusha na magonjwa mbalimbali kiukweli leo
tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na ndio maana unaona wananchi
wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye kisima hiki kwa kuwa
bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.
Wananchi
wao wamemuomba mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir
Mtove kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na
wananchi kwa lengo la kuwatumikia.
Kwa
upande wake mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto
mbalimbali za wananchi kwa kuwa yeye ni mbunge wa wananchi wote bila
kubagua vyama.
Kabati
alisema kuwa ataendelea kuwachimbia visima na kukarabati majengo ya
shule zilizochakaa katika mkoa wa Iringa kwa kuwa yeye ni mbunge wa mkoa
wa Iringa hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kuiamini serikali ya chama
cha mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya kupitia kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli.
“Hivi
hamuoni nimeamua kufika huku ambako hata viongozi wengi hawajafika ila
mimi nimekuja nimewaleta kisima na maji safi na nitaendelea kuja kutatua
matatizo ya mtaa huu kwa kuwa tumetumwa na Rais kufanya kazi kwa
wananchi wa chini ndio maana hata mimi nimeanza kufanya kazi huku mbali
japo kuwa ndio jadi yangu kuwatumikia sana wananchi wa chini sasa
naombeni mniunge mkono katika juhudi zangu za kuwaletea
mandeleo”.alisema Kabati
Aidha
Kabati alisema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuleta
maendeleo kuanzia huku chini kupanda juu hivyo tufanye kazi kwa kujituma
ili tuende sambamba na kasi ya Rais wetu.
Naye
Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove alimshukuru mbunge huyo kwa jihada
zake za kuleta maendeleo na kumuomba kushugulikia changamoto alizozitoa
kwa wananchi ili kuendelea kujijengea imani kwa wananchi wa kata hiyo.Mtove
aliongeza kuwa atahakikisha kata yake inamaliza tatizo la maji ambao
limetumu kwa miaka mingi hivyo wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa
kujituma ili kukuza uchumi wa kata hiyo.
“Angalia
hadi saizi tumechimba visima zaidi ya sita kwenye kata yangu japo bado
sana kumaliza tatizo hili la maji hivyo naendelea kujituma kutafuta
marafiki,wafadhili na kumshirikisha mbunge Kabati kusaidia kutatua
tatizo la maji na changamoto nyingi ili wananchi wangu wafanye kazi kwa
kujituma bila kuwa na vikwazo vyovyote vile vya kiafya”.alisema Mtove.
0 maoni:
Chapisha Maoni