Afisa
Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken akiongea na Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa uzinduzi wa tawi
la benki hiyo jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akikata utepe kuzindua
rasmi tawi la benki ya FNB Tanzania la Arusha huku akiambatana na Mkuu
wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro (wa kwanza kushoto), Afisa Mtendaji
Mkuu wa FNB, Dave Aitken(wa pili kushoto) na Meya wa Jiji la Arusha,
Mh. Calist Bukhai (kulia).
Meneja
wa Tawi la FNB Arusha, Genevieve Massawe akimueleza Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dr. Ashatu Kijaji jinsi mashine ya kisasa ya kuweka
fedha (cash deposit) na kutoa fedha. Mashine hiyo ya kisasa inamuwezesha
mtumiaji kuweka fedha zake benki muda wa masaa 24 imewekwa kwenye tawi
hilo jipya ili kuwawezesha wananchi kuweka akiba fedha zao muda wowote
ule.
Mshauri
wa Huduma kwa Wateja na Mauzo wa FNB Tawi la Arusha, Cecyline Ayo
akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji kuhusu
bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo wakati wa uziduzi
wa FNB Tawi la Arusha mwishoni mwa wiki.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken akimrekebishia kipaza
sati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa
uzinduzi rasmi wa tawi la FNB Tanzania la Arusha mwishoni mwa wiki.
--
First National Bank (FNB) Tanzania imeendelea kupanua wigo wake kitaifa
kwa kufungua tawi jipya eneo la PPF Plaza jijini Arusha kwa lengo la
kuhudumia ongezeko la idadi ya wateja katika mkoa huo.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Dave Aitken
alisema uzinduzi wa tawi la FNB Arusha umelenga kukidhi ongezeko kubwa
la wateja na mahitaji ya huduma za kibenki na kifedha katika kanda ya
kaskazini.
“
Uzinduzi wa tawi la Arusha ni sehemu ya mkakati wa uwekezaji endelevu
uliolenga kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za
kifedha. Pia ni kwa maslahi ya ukuaji wa haraka wa mkoa wa Arusha ambao
una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania” Aitken alisema tawi
la Arusha ni la kumi miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania
ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mitandao ya matawi kwa
kusudi la kuyafikia maeneo mengi ya nchini.
“First
National Bank (FNB), daima tunafikiria njia ambazo zinaweza kutoa
huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la Arusha
litasaidia kuwapatia huduma zote za kibenki wananchi wa mkoa wa Arusha
na wanaoishi maeneo jirani kwani maeneo haya yote yamedhiirika kuwa na
biashara mbalimbali zinazokua kwa kasi,” alisema Aitken.
Akizungumza
kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa tawi hilo, Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema mkoa wa Arusha una uwezo mkubwa wa
kiuchumi na ukuaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kudhihirisha
kuwa mji unakuwa kwa kasi.
“Tunakaribisha
uwepo wa FNB Tanzania Arusha na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha
huduma zenu hapa na mikoa mengine,” Alisema Naibu Waziri. Alisema pamoja
na utajiri mkubwa wa maliasili na utalii, mkoa wa Arusha umechangia
sana katika kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta nyingine za
uzalishaji mali na biashara.
“Arusha
ina fursa na hazina kubwa ya rasilimali jambo ambalo limechangia ukuaji
wa haraka wa biashara katika sekta zote muhimu za kiuchumi. Ni
matumaini yetu uwepo wa FNB katika mji huu utachangia katika kuleta
maendeleo ya biashara kupitia ubunifu wa huduma za kibenki,” Kijaji
alisema.
Vile
vile Kijaji ameitaka sekta ya fedha nchini zimetakiwa kutoa mikopo
inayosaidia wananchi kukuza mitaji yao ambayo kwa sehemu kubwa
itawawezesha katika uzalishaji mali na kuongeza pato lao na nchi kwa
ujumla. Amesema kuwa serikali haiwezi kufanikiwa kutekeleza sera na
mipango yake kwa ufanisi bila kuwepo sekta binafsi hususani sekta ya
fedha hivyo kama serikali inathamini sana mchango wa benki hiyo ya FNB
ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia wananchi wa Arusha.
Tawi
la Arusha lililopo jengo la PPF Plaza linakuja na bidhaa na huduma
mbalimbali zilizobuniwa mahususi kwa ajili ya kuwaongezea tija wateja wa
kawaida na wafanyabiashara katika eneo hili la kanda ya kaskazini.