Posted by Esta Mlibiche on JULY 31,2017 IN NEWS
Mkurugenzi wa kampuni ya Smart
Vision ya Korea, Seo Young Kim (kushoto) na Andrew Chung ambaye ni
mbunifu wa mtambo wa kusafisha maji wakionyesha mtambo huo kwenye
uzinduzi wake kwenye kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani
Monduli Mkoani Arusha
Mkurugenzi wa kampuni ya Smart
Vision ya Korea, Seo Young Kim (kushoto) na mchungaji wa kanisa la
Enyora Daniel Vengei wakiwa kwenye uzinduzi wake katika kitongoji cha
Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
Wananchi wa kitongoji
cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha
wakishuhudia uzinduzi wa mtambo wa kusafisha maji na kuyachuja
uliofanywa na kampuni ya Korea ya Smart Vision.
………………………….
Zaidi ya kaya 700 za wananchi wa
Kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani
Arusha, waliokuwa wanatumia maji ya kwenye bwana wanatarajia kunufaika
na mradi wa kusafisha maji na kuchuja maji kuwa safi uliozinduliwa
Kijiji hapo.
Awali, wananchi hao walikuwa
wanatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kupika, kufua, kuoga na kunywa
maji hayo ya bwawa ambayo pia yalikuwa yanatumiwa na mifugo ya eneo
hilo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Smart
Vision ya Korea, Seo Young Kim akizungumza jana kwenye uzinduzi wa mradi
alisema lengo ni jamii ya eneo hilo kunufaika na maji safi na salama
yanayochujwa kupitia ubunifu wao.
Kim alisema kwa kuanza
kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo, wanatarajia kugawa majiko rafiki ya
mazingira 22 na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji ya bwawa kuwa safi
na salama 22 kwa kaya 22 zitakazowanufaisha zaidi ya watu 220.
Alisema Smart Vision kupitia
uwekezaji wa Korea Trade-Investment Promotion Agency. (KOTRA) jamii ya
eneo hilo itanufaika na na mradi huo wenye lengo la kuondokana na
matumizi ya maji yasiyo safi wala salama ambayo yanasababisha magonjwa
ya tumbo.
“Jamii ya eneo hili kupitia
mchungaji wa kanisa la Enyorata Daniel Vengei, walileta maombi kwetu
kuwa wanatatizo la maji, hospitali na shule, ndipo tukaona tuanze
kutatua hili suala la maji ndipo tukaleta mitambo hii ya kuchuja na
kusafisha maji,” alisema Kim.
She said goal of project, Smart
Vision head about maasai water problem in Korea. Smart Vision developed
water purifier to help maasai people overcome water problem.
Kim said now Smart Vision a Korean
Environmental company launches water project ina Tanzania, hopes to
expand project to other parts of Tanzania where there is lack of
drinking water.
“This project was aided
financially bya KOTRA (Korea Trade-Investiment Promotion Agency) who
supports international business of Korean companies, specifically, the
KOTRA branc in Dar es salaam gave Smart Vision immense support in order
to help people suffering from lack of drinking water though the water
purification project,” said Kim.
She said people who helped with
project is Director of Smart Vision Seo-Young Kim, Manager of Smart
Vision, Hyun-Jung Chung and Purifier developer and volunteer, Andrew
Chung.
Mkazi wa Kitongoji cha Emairete
Rose Lemomo alisema alisema awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la
upatikanaji wa maji safi na salama lakini kupitia mradi huo wataondokana
na maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakiwakabili hasa watoto.
Lemomo aliwashukuru wote
waliohusika na kufanikisha mradi huo, kwani hivi sasa watakuwa wanachota
maji bwawani na kuyachuja na kuyasafisha kupitia mitambo hiyo.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Irmorijo, Mirishi Songoyo alishukuru shirika la Smart Vision kwa
kufanikisha mradi huo wa maendeleo ambao utainufaisha jamii ya eneo hilo
walioteseka kwa muda mrefu juu ya suala la maji.
“Tunawaomba wananchi watakaofikiwa
na mradi huu kuhakikisha wanawasaidia na wale ambao bado wanasubiri
kupatiwa majiko na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji,” alisema
Songoyo.
Mwalimu wa shule ya msingi
Irmorijo, Stephen Laizer aliwataka wananchi wote waliofanikiwa kupatiwa
mradi huo kuhakikisha wanautunza ili kunufaika nao kwa muda mrefu kwani
wameteseka kwa miaka mingi kwenye tatizo la maji.
“Wageni wanapokuja kwenu inawabidi
kuwashukuru hata kama hawajaacha chochote ila hawa wametuletea
teknolojia ya maji, wanaweza kutufanyia mengine mazuri,” alisema
Laizer.
0 maoni:
Chapisha Maoni