Ijumaa, 21 Julai 2017

WANASIASA WAONYWA KUTOLIINGILIA KANISA KATOLIKI

Posted by Esta Malibiche ON JULY 21,2017 IN NEWS
Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea Damiani Dalu akitoa Homilia katika Ibada ya Misa takatifu ya daraja  la upadre  iliyofanyika jana katika kanisa la Bikira Maria Afya ya waonjwa  parokia ya Ilole jimbo katoliki la Iringa.

Na Esta Malibiche Iringa

WANASIASA Nchini wametakiwa kutoliingilia kanisa katoliki kwa kutoa matamko yao
siyo na tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa mapema leo hii na Askofu mkuu wa jimbo kuu  la Songea Damiani Dalu wakati akitoa daraja la upadre  kwa Shemasi Jarome Mtatifikaro  katika kanisa katoliki Parokia ya Bikira Maria mpalizwa Mbinguni Ilole jimbo la Iringa.
Katika homilia yake askofu Dalu alisema kuwa kanisa katoliki halitamvumia mwanasiasa atakaetumia siasa zake kulisemea vibaya na kuwapotosha wananchi kuwa kanisa katoliki linapendelewa kwasababu mh.Rais Magufuli hii si kweli.
"Ndugu zangu wapendwa napenda kuwatahadharisha,kuweni makini na wanasiasa wasiopenda maendeleo ya Nchi yetu wanaodai kutotendewa haki na serikali siasa zao zinadhihirisha kuwa ni kama mchezo wa kuigiza.Mwanasiasa anadiriki  kuchukua  kikundi fulani na kuchochea vurugu ili watu wapigane, Ivi tungewapa nchi nyinyi si Amani tuliyonayo ingepotea kabisa"Alisema Dalu
"""Ninawaomba wananchi muwapuuze wanasiasa hawa ambao hawalitakii mema Taifa letu,ambao wanatumia vyama vyao kumvunja moyo Rais Magufuli.Ninawaomba tuwapuuze na tuungane pamoja kumuombea Rais Magufuli na serikali yake yote ili waendelee kulitete Taifa kwa kutuletea Maendeleo"" Alisema Aakofu Dalu na kuongeza kuwa
Tumeshuhudia wanasisa wakisema Rais Magufuli analipendelea kanisa katoliki hii haikubaliki kabisa.Tumieni siasa kuhamasisha maendeleo na si kuvuruga Amani iliyopo ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
" kwa nini  unatuingilia kwenye dini eti mnatuambia tumekaa kimya hatupambani  na serikali kwasababu inaminya Demikrasia,ni demokrasia gani unayoitaka wewe ivi unatuonaje?Wewe ni nani kama huna dini usikufuru dini zetu Zina heshima yake tena ya kipekee.Tunaomba mtuache na dini zenu na nyie mfanye yenu.
Aidha aliwasihi watanzania kumuunga mkono Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli na kumuombea pamoja na Serikali yake ili waendelee kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
Aidha Askofu Dalu alisema kanisa haliko tayari kupokea wanafunzi wa kike watakaobainika kubeba mimba wakiwa shuleni kuendelea na masomo katika shule zake.
""Hii itasaidia watoto wa kike kuzingatia masomo na kuwa na nidhamu wawapo shuleni.Naipongeza Serikali kwa kuliona hili,nasi shule zetu za kanisa katoliki hatuko tayari kumpokea mwanafunzi atakaebainika kubeba mimba na hatimae kurejea masomoni.
Hata hivyo katika upadrisho huo,parokia ya Ilole ilimkabidhi  zawadi ya gari padre Jarome lenye Thamani ya Tsh.17 Mill.aweze kulitumia katika kutoa huduma ya kanisa hasa vigangoni.


Mhashamu baba Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Songea Damiani Dalu akitoa daraja takatifu la upadre kwa Shemasi Jarome Mtatifikalo aliyelala kifudifudi.




Mhashamu baba Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Songea Damiani Dalu akitoa daraja takatifu la upadre kwa Shemasi Jarome Mtatifikalo aliyelala kifudifudi.


Padre Jarome Mtatifikalo akiwa amelala kifudifudi kuonyesha utii huku litania ikiimbwa
Mhashamu baba aakofu mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Songea akimuwekea mikono kichwani Padre Jarome Mtatifikalo mara baada ya kupata daraja takatifu la upadre 


Padre Jarome Mtatifikalo akiwa akmisikiliza kwa makini mhashamu baba Aakofu mkuu Damiani Dallu (hayupo pichani)mara baada ya kupewa daraja takatifu la upadre.


Mapadre wakimuwekea mikono kichwani padre Jarome Mtatifikalo 


Mapadre wakimuwekea mikono kichwani padre Jarome Mtatifikalo




Padre Jarome akivalishwa vazi rasmi la kipadre.





Mapadre mbalimbali kutoka jimbo katoliki la Iringa na nje wakishiriki


Mhashamu baba askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea Damiani Dalu akibariki gari ambalo ni zawdi aliyokabidhiwa padre Jarome.





















0 maoni:

Chapisha Maoni