Alhamisi, 13 Julai 2017

MAVUNDE AZINDUA MPANGO WA URASIMISHAJI UJUZI KWA VIJANA KIGOMA

Na Esta Malibiche on JULY 13, 2013 in KITAIFA

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu Mhe ANTHONY MAVUNDE akizungumza na wananchi wa Mkoa waKigoma  katika moja ya ziara aliyoifanya mkoani humo.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu Mhe ANTHONY MAVUNDE akizungumz na wananchi wa Mkoa waKigoma  katika moja ya ziara aliyoifanya mkoani humo,kushoto kwake ni Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Zuberi Kabwe kupitia chama cha ACT wazalendo.









Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Kazi, Na Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu *Mhe ANTHONY MAVUNDE* amezindua mpango wa Urasimishaji wa Ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo Rasmi wa Mafunzo kwa vijana wa Kanda ya Magharibi Mkoani Kigoma na kuwataka vijana kujitokeza kuchangamkia fursa za Mafunzo zinazotolewa na Serikali ili waweze kushiriki katika kujenga Uchumi imara kupitia Mapinduzi ya Viwanda.

MAVUNDE amesema Serikali imetenga fedha za kutosha kugharamia mafunzo kwa Vijana  elfu tatu Mia tisa 3,900* katika maeneo mbalimbali nchini hatua ambayo itawasadia kuwajengea uwezo vijana  kushiriki kikamilifu katika Maendeleo ya Taifa kupitia Mapinduzi ya Viwanda ambapo baada ya mafunzo hayo Vijana watatambuliwa rasmi kwa kupewa vyeti vya Mafunzo Ufundi kutoka VETA bila ya wao kusoma na kufanya mitihani katika utaratibu.Mavunde amewaasa Vijana hao watakaopatiwa mafunzo hayo kutumia elimu hiyo kama msingi wa kujiajiri na kujitegemea na pia mafunzo hayo yatumike kama chachu katika uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati.

Awali akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa Mpango huu, Mbunge wa  Viti Maalum wa CCM Mkoa wa Kigoma Mh Josephine Genzabuke amempongeza Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake kwa ujumla kwa Mpango huu wa kuwajengea Vijana ujuzi unaolenga katika kuwafanya Vijana waweze kutambuliwa rasmi na kujiajiri.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini *Mhe Zitto Zuberi Kabwe* ameipongeza Serikali na kumshukuru Mh Mavunde kwa kuzindua Mpango huu utakaosaidia Vijana wa Tanzania katika kutatua changamoto ya ukosefu wa Ajira kwa kuwaandaa kujitegemea na kujiajiri.

Mhe Zitto amesema katika uchumi wa Sasa wa Dunia nguzo pekee kwa vijana kufanikiwa baada ya Kupewa Mafunzo ni kujiunga katika vikundi vya umoja ili waweze kufikiwa kwa haraka na Serikali katika kupatiwa Mikopo na fedha zinazotengwa kwa ajili ya makundi ya vijana,na wanawake itakayowasaidia kujiajiri wenyewe.

Mpango huu unafadhiliwa kwa asilimia Mia moja na Serikali na unatekelezwa kwa pamoja na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi - *VETA,* ambapo kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo wa VETA *Bi. Leah Lukindo* amewahakikishia vijana kuwa watatumia mtandao wa vyuo vya *VETA* kuwafikia vijana ambao ndio walengwa wa kuu wa mpango huo katika maeneo mbalimbali nchini.

*Imetolewa na Idara ya Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu.*
*13/07/2017*

0 maoni:

Chapisha Maoni