Jumatano, 26 Julai 2017

MKUU WA WILAYA YA MBULU CHELESTINO MOFUGA AWATAKA WAKUU WA SHULE KUSIMAMIA NIDHAMU

Posted by Esta Malibiche on JULY 26,2017 IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Mbulu,Chelestino Mofuga akizungumza mapema leo hii na Wakuu wa shule na Maofisa Elimu  wa wilaya ya Mbulu.

Mkuu wa wilaya ya mbulu Chelestino S MOFUGA Leo 26/7/2017 amekutana na wakuu wa shule za msingi wilaya nzima, maafisa elimu kata, wathibiti ubora wa shule na maafisa elimu wote ikiwa ni siku moja tu tangu kampeni ya kuzuia mimba za wanafunzi kuzinduliwa jana ikiwa na kauli mbiu Mbulu bila mimba za wanafunzi inawezekana, tuache wanafunzi wa kike wasome. 
Mofuga amewaagiza wakuu wa shule na watumishi wa elimu, kwamba wanatakiwa kusimamia nidhamu za wanafunzi na watumishi, na kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria masomo kikamilifu.  

Pia amewataka  kampeni ya kuzuia mimba za wanafunzi iwe wimbo wa shule wa kila siku wanapofanya matangazo kwa wanafunzi na mikutano ya wazazi, na kila shule lazima ibandike bango la kuzuia mimba shuleni hadi madarasani na ofisi zote za Shule, Halmashauri  na za vijiji.

  Maagizo mengine waliyopewa ni kusimamia ufundishaji ili kufikia malengo ya asilimia 80 ya ufaulu. Pia kila shule inatakiwa kuunda timu ya wakaguzi wa ndani,  kamati za taaluma na zinatakiwa kufanya kazi kikamilifu, taarifa ya ufundishaji ya kila mwezi lazima ifike wilayani ambapo pia kuna timu ya maafisa elimu kata watakaofanya kazi kama sekretarieti ya elimu ya wilaya na watachambua ufundishaji wa kila mwezi.

 Aidha amesisitiza kuwa  mkuu wa shule ambaye hatasimamia kikamilifu taaluma na kampeni ya kuzuia mimba za wanafunzi atakuwa hatoshi kuwa mkuu wa shule.













0 maoni:

Chapisha Maoni