Na Esta Malibiche
Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela amewataka wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuwajali watoto wenye
ulemavu kwa kuwapa haki wanazostahili kama watoto wengine.
Kauli hiyo ameitoa mapema leo hii wakati akizungumza
na wazazi na watumishi wa kituo cha kulea watoto wenye ulemavu cha Ali Nyumba kilichopo eneo la Wilolesi Manispaa ya Iringa.
Kasesela akiwa kituoni hapo alisema kumekuwa
na wimbi kubwa la baadhi ya wazazi na walezi kuwaficha ndani watoto wenye
ulemavu huku wengine wakiwanyanyasa na
kutowapa haki stahiki kama watoto wengine jambo ambalo halistahili katika jamii.
“ Nasikitishwa na baadhi ya wazazi
na walezi amabaowanawaficha ndani watoto
wenye ulemavu na wengine wanadiliki kuwatelekeza na kuwatupa bila kujali utu hili
halikubaliki.Pia nachukia sana tabia ya baadhi ya akina baba kukimbia watoto
wenye ulemavu na kuwachia akina mama kulea peke yao.’’Alisema Kasesela na
kuongeza kuwa
Aidha aliwataka maofisa tarafa wafanye
utafiti nyumba hadi nyumba kubaini kama kuna mtoto mlemavu,sababu baadhi ya
wazazi huwa wanawaficha watoto wao ndani hivyo kuwasababishia kukosa haki zao
za msingi.
Awali akisoma taarifa ya kituo hicho
mbele ya Mkuu wa Wilaya, mratibu wa kituo hicho Bwana Adam Duma alisema lengo
la kuunda umoja huu ulikuwa ni kuwakutanisha wazazi ili waweze kuwa na sauti
moja katika kubainisha na kusaidiana katika kutatua changamoto mbalimbali
zinazo ikumba jamii ya watoto waishio na ulemavu.
Duma alisema kituo cha Ali Nyumba kinaendeshwa
kwa msaada wa wahisani mbalimbali ambapo
mahitaji makubwa ni pamoja na chakula, baiskeli za walemavu pamoja na gharama
za uendeshaji.
‘’Mheshimiwa Mkuu wa Wialaya tumefungua
vituo viwili, kimoja kipo hapa wilollesi na kingine Ngome,ambapo Kituo kimoja
kinapokea watoto 35.Vituo hivi vinawasaidia watoto wenye ulemavu wa viungo na
mtindio wa ubongo kwa kufanya mazoezi ya viungo pamoja na kuwafundisha kazi za
mikon’’Alisema Duma.
Katika kituo hiki yupo mtoto aitwaye
Zawadi ambaye amesomeshwa hadi kiwango cha darasala saba, Mtoto huyu hawezi
kutumia mikono anatumia miguu kwa shida akisaidiwa na kompyuta na amefanikiwa
kuandika kitabu kinacho elezea maisha yake’’Alisema Duma.
Bi.Naumi
Patrick ni Mmoja wa wazazi wa watoto wenye ulemavu nae aliwasihii
wazazi wenzie kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu huku akiitaka
serikali iingilie kati kwa mzazi atakaebainika na vitendo vya kikatili
na unyanyasali dhidi ya watoto wenye ulemavu
''Kuna
baadhi ya wanaume na familia wamekuwa na fikra potofu na kuona kuwa
mtoto mlemavu ni Mkosi katika familia hivyo wanatutelekeza na kutuacha
tukilea peke yetu.Sisi tumeona tuungane na kutetea haki ya watoto wetu
maana nao wanastahili kupata haki sawa na wengine kama Elimu na Mahitaji
muhimu'''Alisema na kuongeza kuwa
''Ninawaomba
wazazi wenzangu tusiwafiche watoto wenye ulemavu.Tu jitokeze kupinga
huu unyanyasaji dhidi ya vitendo wanavyofanyiwa watoto wenye ulemavu na
tuwafichuewale wote wanaowaficha watoto wenye ulemavu ndani''Alisema
Bi.Naumi.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni