Posted by Esta Malibiche on JULY 31,2017 IN NEWS
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi
Sihaba Nkinga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya
Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi
katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa
Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na
washiriki wa mkutano wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kabla ya
kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo ya
Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo
yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro
leo 31.7.2017.
Mkuu
wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo
(kulia) Bw. Paschal Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya
kudhibiti viashiria hatarishi kabla ya kukaribisha Katibu Mkuu wa Wizara
ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga
(katikati) aweze kufungua mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala
wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi kutoka vyuo vya
Maendeleo ya Jamii vinavyosimsmiwa na Wizara wakifuatilia kwa makini
mazungumzo ya Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa uendeshaji wa
mafunzo hayo katika ukumbi wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo
31.7.2017.
Watendaji
kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kutoka kulia ni Mkurugenzi Utawala na
Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu Bibi Deodata Makani ,
katikati ni Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi Bibi Martha chuma na kushoto
ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bibi Lightness Mchome wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi
Sihaba Nkinga(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti
wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika
katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo
31.7.2017.
Mkurugenzi
Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu kwa kutoka Wizara
ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani
akitoa somo juu ya masuala ya kuzingatia kwa Wakuu wa Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa
Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika
Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo
cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni mwenyekiti wa mafunzo Bw.
Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria
Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya Jamii
yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro
leo 31.7.2017.
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto akiwasilisha mada kuhusu uaandaaji mzuri wa Bajeti kwa
Wakuu wa Vyuo vua Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo ya ya
Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo hao
yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro
leo 31.7.2017.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bibi Sihaba Nkinga (katikati waliokaa)akiwa akiwa na wakufunzi wa vyuo
vya Maendeleo ya Jamii nchini wakati wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria
hatarishi mahala pa kazi yaliyofanyikakatika Ukumbi wa Mbegu za miti,
mkoani Morogoro leo leo 31.7.2017. Picha na Erasto Ching’oro WAMJW
Na Erasto Ching’oro WAMJW.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika
utendaji wao wa kazi katika kuendesha vyuo wanavyovisimamia.
Ameyasema
hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu udhibiti wa
viashiria hatarishi vya utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na
kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa
kila siku ili kuepuka hoja za ukaguzi wa fedha.
Amesisitiza
kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi
mahala pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi
wa Umma katika kutimiza majukumu yao.
“Niwatake
Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu
zilizopo katika kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika
suala la udhibiti wa Fedha katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.
Aidha,
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya
maalum, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za
ukaguzi mahala pa kazi kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili,
maarifa na miongozo na weledi unaotakiwa katika uendeshaji wa vyuo.
Aidha
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wakuu wa vyuo kuongeza umakini
katika utekelezaji wa majukumu yao mahala pa kazi, kuimarisha
mawasiliano katika uwajibikaji wa pamoja kwa kuimarisha mifumo ya
utendaji kazi katika vyuo vya maendeleo ya jamii.
Mafunzo
haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na
Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na kushirikisha vyuo vya Buhare,
Uyole, Rungemba, Ruaha, Mabughai, Monduli na Mlale.
0 maoni:
Chapisha Maoni