Posted by Esta Malibiche on JULY 27,2017 IN NEWS
Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo wananchi hao walipigwa na duwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo kubwa la kijiji ilikuwa ni changamoto kubwa na iliyodumu mrefu hali iliyopelekea wananchi kutumia maji ambayo si safi na salama.
Wananchi wengi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.
"" Ni matumaini yangu kwamba ile adha kubwa ya upatikanaji wa wa maji katika eneo kubwa la kijijini Matumbulu itaisha na kusaidia wanakijiji kupata maji safi na salama kwa wakati"Alisema Mavunde
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Mh Emmanuel Chibago amempongeza Mbunge Mavunde kwa anavyojitoa kuwatumikia wanadodoma na kuwaletea maendeleo na hivyo kuwaomba wanadodoma wampe ushirikiano ili afanye makubwa zaidi.
Nakuomba uwe makini na issue ya typing mara kadhaa nasoma humu naona unakosea kuandika tafadhari.
JibuFuta