Posted by Esta Malibiche on JULY 25,2017 IN NEWS
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akizungumza na wanafunzi wa kike wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupima mimba kwa wanafunzi wa kike zilizopo wilayani humo. |
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino S MOFUGA Leo 25/7/2017 amezindua kampeni ya kuwapima mimba wanafunzi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli kuhakikisha hakuna wanafunzi wajawazito na waliozaa kuendelea na masomo katika mfumo wa kawaida yaani formal education.
Zoezi la uzinduzi wa kampeni hiyo aliyopewa jina la MBULU BILA MIMBA ZA WANAFUNZI yawezekana, TUACHE WATOTO WA KIKE WASOME! Mkuu wa wilaya amewagiza wakurugenzi na wakuu wa shule kupima wanafunzi kila baada ya miezi mitatu, na amewambia wanafunzi atakayepata mimba amejifukuzisha shule mwenyewe kwani serikali haina mpango wa kusomesha wanafunzi wajawazito na wazazi.
Pia amewaonya walimu na wananchi wanaotembea na wanafunzi kwamba wakibainika watakwenda jela miaka 30 bila HUDUMA .
Aidha amewataka walimu wakuu kusimamia taaluma na nidhamu na kuwafichua wazazi wanaokwamisha maendeleo ya wanafunzi shuleni kwa kuwatuma kuchunga Ngombe siku za shule au kufanya biashara na wazazi wanaoficha wahalifu wa mimba au kukubaliana kuwaozesha.
0 maoni:
Chapisha Maoni