Posted by Esta Malibiche on JULY 31,2017 IN BIASHARA
SERIKALI ya Tanzania,
imeshukuru Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) kwa kuwezesha
watanzania kupambana na umaskini kupitia miradi wanayoidhamini au
kuitafutia fedha.
Kwa miongo miwili UNCDF imekuwa
ikifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya
rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) katika mpango wa
kupeleka madaraka kwa umma na shughuli za maendeleo ya kiuchumi .
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa
Iyombe katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala wa mkoa wa
Kilimanjaro Aisha Amour kwenye ufunguzi wa kongamano la siku 2 la Wadau
wa Ufugaji Samaki Kibiashara Bwawa la Kalemawe lililoko wilaya ya Same
mwishoni mwa wiki.
“Tunafurahishwa kwa namna ya
pekee na UNCDF kwa jitihada zake zinazoendeshwa kupitia katika Mpango wa
Ufadhili Miradi ya kiuchumi (LFI),” alisema Iyombe na kuongeza:
“Tunapokutana hapa tunapewa
fursa na kufunuliwa uzoefu wa ushiriki wa UNCDF katika miradi
mbalimbali, safari hii tukishuhudia hatua yake ya kushirikiana na
Halmashauri ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro.”
Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo
kuhusu mradi wa ufugaji samaki katika shamba hilo kwa viongozi
mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi ya mafunzo juu ya
ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya
Bagamoyo. Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mh. Naghenjwa
Kaboyoka na Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Staki
pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (wa pili kulia).
Pamoja na kushukuru kwa hatua
mbalimbali zilizofikiwa na taasisi hiyo katika kusaidia watanzania,
aliwataka wakazi wa Same kuhakikisha kwamba mradi huo ulioundiwa kampuni
ili kwenda kibiashara unafanikiwa na kuwa mfano kwa wengine.
Halmashauri ya wilaya ya Same, na
jamii inayozunguka bwawa la Kalemawe wanashirikiana na UNCDF kuboresha
miundo mbinu ya bwawa hilo na kuwezesha uwapo wa uwekezaji kwa kuanzisha
kampuni.
Kampuni hiyo iliyosajiliwa ya
Kalemawe Dam Investment Limited katika mpango maalum (SPV) inamilikiwa
na wadau mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Same, halmashauri
ya vijiji sita, wakala wa serikali, watu binafsi pamoja na makundi ya
kijamii.
Kuwapo kwa kampuni hiyo ni juhudi
zinazofanywa za kuwezesha uhusiano mahsusi wa kibiashara unaohusisha
ubia wa Serikali, Binafsi na jamii (PPCP) kwa kutoa umiliki linganifu
mpaka katika ngazi za chini za mamlaka za kijiji, ambazo kimsingi ndizo
wamiliki wa maliasili muhimu ya ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya
Vijiji ya Mwaka 1999.
Viongozi
mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) wakiwa kwenye ziara fupi ya mafunzo
kuhusu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba la ufugaji samaki la
Ruvu lililopo wilaya ya Bagamoyo.
Mradi huo wa Ufugaji wa Samaki
Kibiashara wa Bwawa la Kalemawe ni zao la ushirikiano kati ya
Halmashauri ya Wilaya ya Same, Kata za Ndungu na Kalemawe, asasi zisizo
za kiserikali na wadau wa maendeleo walioazimia kukarabati na kufufua
bwawa hilo na mfumo wake wa kilimo cha umwagiliaji.
UNCDF kwa kushirikiana na wabia
wake waitwao Mikono Tayari (ambao ni kundi linaloundwa na washirika
kutoka Tanzania na Norway) ni wataalamu katika mradi hu wa ufugaji
samaki kwa pamoja na SPV ya Same na washirika wake.
Katika kongamano hilo Mkuu wa
wilaya ya Same Rosemary Staki amesema wilaya yake ipo tayari kutekeleza
mradi huo ambao una manufaa makubwa si tu kwa watu wa Kalemawe na vijiji
vinavyozunguka bali pia na halmashauri ya wilaya ya Same.
Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo
kuhusu vyakula vinavyotumika kulisha samaki wanaofugwa kwenye shamba
hilo kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi
ya mafunzo juu ya ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo
lililopo wilaya ya Bagamoyo.
Akishiriki katika mjadala
aliwataka wanakalemawe kutambua umuhimu wa mradi huo na kwamba hicho ni
kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa watu binafsi na jamii kwa ujumla.
Mradi huo ambao ni sehemu ya
programu kubwa ya kubadili watu wenye makazi kuzunguka bwawa hilo
umelenga katika siku za usoni kuzalisha samaki na vifaranga vyake.
Ili kuwa na uelewa mkubwa wa
kufanya biashara hiyo ya samaki, madiwani na wenyeviti wa serikali za
mitaa za vijiji vinavyotengeneza kampuni hiyo ya Kalemawe walitembelea
shamba la samaki Ruvu ambapo waliona shughuli mbalimbali zinazoendelea
katika shamba hilo ili iwe mfano kwao
Pamoja na kuuza samaki shamba hilo
ambalo lipo kilomita 20 kutoka Bagamoyo na kilomita 13 hivi kutoka
Mlandizi linafuga samaki aina ya sato na hutotolesha vifaranga laki moja
kila wiki kwa kulingana na oda zilizopo.
Ziara
ya mafunzo ikiendelea katika shamba la kufuga samaki la Ruvu lililopo
wilayani Bagamoyo. Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (wa pili
kushoto) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (katikati) pamoja na ujumbe
ulioambatana nao kwenye mafunzo hayo ukitazama jambo katika shamba hilo.
Mmoja wa viongozi katika mradi huo
Khumbo Kanthenga alisema kwamba mradi huo ambao bado unapanuliwa
kufikia mabwawa sitini kwa sasa umelenga kutoa vifaranga kwa mujibu wa
oda na pia kuuza samaki ambao wapo tayari kuingia sokoni samaki hao
wanafikia gramu 350 na kuendelea.
Naye Mbunge wa Same Mashariki,
Naghenjwa Kaboyoka ambaye alikuwapo katika kongamano hilo alielezea haja
ya wananchi wengi kutambua mipaka yao na kuhakikisha kwamba dhamira
safi iliyopo ya kufufua bwawa hilo na kubadilisha maisha ya wananchi
inafikiwa.
Wakifunga Kongamano hilo UNCDF ili
shukuru ushirikiano mkubwa wa karibu ambao umeonyeshwa na washiriki wa
warsha hii ya wadau kuanzia serikali kuu, mkoa, willaya na viongozi wa
vijiji sita vinavyohusika na utekelezaji wa mradi na pia iliahidi kua
mashirika mengine ya umoja wa mataifa watashirikishwa kuwa sehemu ya
utekelezaji wa mradi huu na miradi mingine mbalimbali katika eneo hili
la bwawa la samaki.
Eneo
ambalo linaandaliwa kwa ajili ya bwawa la kufugia samaki katika shamba
la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamayo.Wafanyakazi
wa shamba la kufugia samaki la Ruvu wakitega nyavu kwa ajili ya
kuonyesha samaki katika moja ya mabwawa kwenye shamba hilo wakati wa
ziara hiyo fupi ya mafunzo.Mmoja wa wafanyakazi wa shamba hilo akiwa ameshikilia samaki aina Sato wanaofugwa kwenye shamba hilo.Meneja
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (tisheti nyekundu) akitoa
maelezo katika chumba maalum cha kutotolea vifaranga vya samaki kwa
viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliokuwa kwenye ziara fupi ya
kupata elimu juu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo
lililopo wilaya ya Bagamoyo.Mshauri
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Per Gjoede akitazama mabwawa ya samaki
katika shamba la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamoyo.Mkurugenzi
wa Shamba la Samaki la Ruvu, Daudi Makobole (wa pili kulia)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (kulia)
pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya
Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (kushoto), Mshauri wa Shamba la
Samaki la Ruvu, Per Gjoede (wa pili kushoto) baada ya kuhitimisha ziara
fupi ya mafunzo katika shamba hilo.Mkuu
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)
nchini, Peter Malika akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam.Mgeni
rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour
akizungumza wakati ufunguzi wa warsha ya siku mbilli ya wadau wa mradi
wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Same, Rosemary Staki.Mkuu
wa wilaya ya Same, Rosemary Staki akitoa salamu kwa wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe wakati wa warsha
hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Ofisa
Mwandamizi anayeshughulikia uwekezaji katika Shirika la Umoja wa
Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), Imanuel Muro akisimamia
majadiliano kuhusu wa kampuni ya bwawa la Kalemawe lililopo wilayani
Same mkoani Kilimanjaro wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi
wa ufugaji samaki kibiashara katika bwawa hilo iliyoandaliwa na UNCDF
na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Mkiurugenzi
Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dr. Charles Mhina
akitoa maoni kwenye warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti
wa kijiji cha Misufini kata ya Ngungu wilaya ya Same, Omari Mganga
akiwasilisha maoni wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti
wa kijiji cha Mgandu kata ya Bendera wilaya ya Same, Merina Mhando
akichangia maoni katika warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa
ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Mtaalamu
wa Mawasiliano na Ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko
wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini, Jacqueline Namfua-Mwombela na
Mshirika wa Programu UNCDF, Andulile Mwabulambo wakifurahi jambo wakati
wa warsha hiyo iliyofanyika wmishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Pichani
juu na chini ni washirki wa warsha ya siku mbili ya mradi wa ufugaji wa
samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyoandaliwa na UNCDF na
kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni