Posted by Esta Malibiche on JULY 10,2017 IN NEWS
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka |
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi usiku wa Julai 8,2017, amezindua rasmi tamasha la
Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), tukio lililofanyika Ngome Kongwe,
Mjini Unguja-Zanzibar.
Katika
tukio hilo, Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la 20,
tokea kuanzishwa kwake miaka 20, iliyopita. Ambapo uongozi wa ZIFF waliweza
kusoma wasifu wa Rais huyo Mstaafu kwa namna alivyoweza kusaidia mchango mkubwa
kuendeleza tasnia ya filamu nchini na
sanaa kwa ujumla huku akiwa ndio kiongozii wa juu kabisa hapa nchini kuizungumzia
mara kwa mara tamasha hilo la ZIFF.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmo, Dkt. Jakaya Kikwete alishukuru na kupongeza kwa
mafanikio waliyopata ZIFF hadi kufikia msimu wa 20, tokea kuanzishwa kwake
ambapo imewataka waendelee zaidi na zaidi.
“Nashukuru
kwa kunialika. Nashukuru kwa tuzo hii kwani sikutegemea na nina wapongeza kwa
mafanikio haya ua kutimiza miaka 20. Nawaombeeni muendelee miaka 20 na 20 zaidi vizazi na vizazi mpaka litakapofika
mwisho” alieleza Dkt. Kikwete.
Dkt.
Kikwete alitoa ushahuri kwa uongozi wa ZIFF kuwa na kifua mbele kwa namna
filamu zinazopita kwenye tamasha lao
kuzifuatilia kwani zimekuwa zikifanya vizuri huko mbele ikiwemo tuzo za Hollywood.
Kwani ZIFF imekuwa ni taasisi yenye nafasi muhimu kwa
jamii ya watu wa Zanzibar Tanzania . Kwa
sasa ni kujipima katika miongo miwili hii ni jinsi gani na kiasi gani ZIFF
ilivyojisogeza na kuwa karibu na jamii” alieleza Dkt. Kikwete.
Aidha,
Dkt. Kikwete alieleza kuwa, tasnia ya sanaa hapa nchini inatakiwa ipande na
kuwa juu ili kuendeleza utamaduni wa Mzanzibar na Mtanzania inaenda vipi. Pia
amewataka ZIFF kuwa karibu na jamii ili kuweza kujenga ushawishi kwa jamii hiyo
na kilamwaka wawe na matamanio zaidi ya tamasha.
Awali
akitangaza tuzo hiyo, Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo mbele ya jopo la wajumbe wa Bodi ya ZIFF,
waliweza kumtangaza rasmi Dkt. Kikwete kutwaa tuzo hiyo kubwa kabisa ambayo
utolewa kwa watu wenye kutukuka ambao pia wameifanya mchango mkubwa ndani na
nje katika masuala ya Sanaa na tasnia ya filamu.
Mwenyekiti
wa ZIFF Mahmoud Thabit Kombo aliweza kuwataka wazawa hasa Wazanzibar kuwa na
mwamko wa kuthamini cha kwao na hata kujitokeza kudhamini tamasha hilo.
“ZIFF
imefungua milango yake wazi kwa mtu yeyote kujitokeza na kudhamini tamasha
hili. Wazawa tunawakaribisha sana kwani
uwepo wa tamasha ili ndio kukuwa kwa uchumi wetu na maendeleo hivyo tujisikie
fahari kwa uwepo wake”. Ameeleza Mahmoud Thabit Kombo.
Akiwa
mgeni rasmi, Dkt. Kikwete aliweza kushuhudia filamu ya uzinduzi wa tamasha hilo
ya ‘T-Junction’ iliyoandaliwa na mtayarishaji wake Amir Shivj kutoka Kijiweni Production ya Dar es Salaam.
Katika
uzinduzi huo, Ngome Kongwe iliweza kufurika umati mkubwa waliojitokeza
kushuhudia uzinduzi huo.
Imeelezwa
kuwa, wageni kutoka mataifa mbalimbali zaidi ya 14,000 wamefika Visiwani
Zanzibar huku hoteli mbalimbali zikiwa zimepata faida kwa kipindi hiki,
alieleza Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo ambapo ameweka wazi kuwa katika
orodha yao ya wageni kutoka Mataifa mbalimbali huku wengine wakiendelea kufika
kila siku.
Tamasha
hilo linatarajia kumalizika hadi Julai 16,2017. Huku kila siku kukiwa na filamu
zinazoonyeshwa Ngome Kongwe na zingine zikioneshwa kwenye kumbi mbalimbali
ndani ya viunga vya Unguja pamoja na Vijiji vya Zanzibar sambamba na kutoa mafunzo
ya uendeshaji wa filamu na mafunzo mbalimbali katika tasnia hiyo ya filamu.
Imeandaliwa na Andrew Chale, MO BLOG-Zanzibar
Mkurugenzi
wa ZIFF, Daniel Nyalusi (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Zanlink
wakipata picha wakati wa ufunguzi huo wa tamasha la ZIFF 2017, ambalo
kwa mwaka huu ni la 20, tokea kuanzishwa kwake.
Wadau
mbalimbali wa wakipata picha wakati wa ufunguzi huo wa tamasha la ZIFF
2017, ambalo kwa mwaka huu ni la 20, tokea kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi
wa zamani wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akijadiliana jambo na
Mkurugenzi wa Busara Promotion ambao ni waandaji wa tamasha la Muziki la
Sauti za Busara, Yusuph Mahmoud ama 'Dj Yusuf'
wadau wakiwa kwenye picha ya kumbukumbu
Mwendesha kipindi cha senema zetu akiwa 'mbashara' wakati wa ufunguzi huo
Mmoja
wa wageni waliofika kwenye tamasha hilo ambapo alikuwa kivutio kwa
muonekano wake wa kama aliyeigiza filamu ya YESU " JESUS'
Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabiti Kombo akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa ZIFF, Daniel Nyalusi wakati wa uzinduzi huo
Mmoja
wa wadau wakubwa wa tasnia ya filamu na muziki hapa nchini Dada Sauda
Simba akihojiwa 'mbashara' na kipindi cha SINEMA ZETU
Wadau mbalimbali wakipata picha ya ukumbusho kwenye zuria jekundu
wadau wakipata kumbukumbu
Mkurugenzi
wa Fabrizio Colombo akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Busara
Promotion ambao ni waandaji wa tamasha la Muziki la Sauti za Busara,
Yusuph Mahmoud ama 'Dj Yusuf'
Burudani ikiwendelea
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa zamani wa ZIFF, Profesa Martin Mhando
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi wageni
waalikwa wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongzi wengine
wakipiga makofi kupongeza bendi iliyokuwa ikitumbuiza
upande wa viongozi na wagei waalikwa wakifuatilia tukio hilo
Wakurugenzi
wapya wa ZIFF wakitambulishwa katika ufunguzi huo, kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa ZIFF Daniel Nyalusu na kushoto ni Mkurugenzi wa
ZIFF Fabrizio Colombo
Mkurugenzi wa ZANLINK akizungumza katika tamasha hilo
Burudani
Mwenyekiti wa ZIFF 2017, Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Kikwete jukwaani
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshika tuzo yake hiyo
ya mtu aliyetukuka wa ZIFF baada ya kukabidhiwa na Bodi ya ZIFF usiku wa
Jumamosi Julai 8,2017. Ngome Kongwe, Unguja
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika tukio hilo
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatilia filamu ya
T-Junction ya Amri Shivji iliyokuwa ikifungua tamasha hilo
Dkt.
Kikwete akiselebuka pamoka naMkurugenzi wa ZIFF, Fabrizo Colombo pamoja
na kikundi cha Mwandege wakati wa tukio hilo la ufunguzi wa tamasha la
ZIFF la 20
Mkurugenzi wa ZIFF, Fabrizo Colombo akizungumza katika tukio hilo
Amir Shivj wa Kijiweni Production akitambulisha 'crew' yake ya wasanii walioigiza katika filamu ya T-Junction.
Picha zote na Andrew Chale-MO BLOG, Zanzibar
0 maoni:
Chapisha Maoni