Ijumaa, 28 Julai 2017

MOFUGA AWATAKA WANANCHI KUWEKEZA KATIKA ELIMU WILAYANI MBULU

Posted by Esta Malibiche on JULY 27,2017 IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya utafiti wa Ten/Met  inayohusu ushieika wa wadau wa Elimu wilayqni Mbulu.
Mkuu wa wilaya ya mbulu  Chelestino S MOFUGA  Leo  27/7/2017 amezindua ripoti ya utafiti wa Ten/Met kuhusu ushiriki wa wadau wa elimu katika kupanga bajeti na utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya elimu   mkuu wa wilaya  amewapongeza sana Ten/Met nakuwambia utafiti huo utatumika kuboresha utendaji wa serikali wa kila siku.  
Aidha amewambia mbulu ipo nyuma katika elimu na wilaya nzima haina chuo kikuu, hivyo anakaribisha wadau wanaotaka kuwekeza katika chuo ambapo wilaya imetenga ekari 300 kwa mradi huo. 







0 maoni:

Chapisha Maoni