Posted by Esta Malibiche on JULY 10,2017 IN SIASA
Katibu
wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Iringa (UVCCM) James Mgego (pichani)
amewahimiza vijana wa jumuiya hiyo kujitokeza kugombea nafasi za uongozi
hasa wasichana ambao wako nyuma kuchangamkia fursa hizo.
Akizungumza na mtandao huu wa Habari mapema leo hii alisema kuwa tangu kuanza kwa zoezi hilo ngazi ya
mkoa ni vijana 44 tu kati yao wakina dada ni wanne, ikizingatia kuwa
mwaka 2017 wa uchaguzi ndani CCM.
Mgego
alisema kuwa jumuiya hiyo ni jumuiya ya vijana ya CCM ni kwa ajili ya
vijana wote wakiume na wakike lakini inashangaza kuona dada zetu
wanakuwa nyuma kuchangamkia fursa za kugombea nafasi za uomgozi ndani ya
umoja huo.
Pia
katibu huyo aliwataka vijana kuendelea kujitokeza kuchukua fomu za
kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na kutowasikiliza
watu ambao wapo kuona CCM inakwama katika uchaguzi huo wa ndani ya
chama.
Alisema
kuwa zoezi la utoaji fomu za uongozi wa UVCCM ngazi ya mkoa ilianza
tarehe 02.07.2017 na kukamilika tarehe 10.07.2017 katika ofisi ya UVCCM
mkoa wa Iringa na katika ngazi ya wilaya zoezi pia linaendelea na
kuongoza kuwa fomu hizo zinatolewa bila malipo.
Mgego
alizitaja nafasi hizo za uongozi zinagombewa kuwa ni mwenyekiti UVCCM
Mkoa, Mjumbe wa mkutano Mkuu CCM Taifa, Mjumbe Baraza Kuu UVCCM, Mjumbe
Mmoja Kuwakilisha UWT, Mjumbe Mmoja kuwakilisha Wazazi, Mjumbe wa
Mkutano Mkuu CCM Mkoa na Mjumbe wa mkutano wa UVCCM Taifa.
“Tulianza
na uchaguzi wa mashina umekamilika, ukafuata wa ngazi ya kata
naomemalizika na vikao vyake vinaendelea kuchuja wagombea na sasa ni
uchaguzi wa UVCCM ngazi mkoa na taifa unaendelea…”alisema katibu huyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni