Alhamisi, 27 Julai 2017

MBUNGE WA DODOMA MJINI ANTHONY MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU

Posted by Esta Malibiche on JULY 27,2017 IN NEWS

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mh Anthony Mavunde leo amekamilisha ahadi yake katika kijiji cha Matumbulu kwa kutoa mabomba ya kutandazia maji kijiji kizima yenye urefu wa Km 1 na yenye thamani ya zaidi ya Tshs 8m.

Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo wananchi hao walipigwa na duwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo kubwa la kijiji ilikuwa ni changamoto kubwa na iliyodumu mrefu hali iliyopelekea wananchi kutumia maji ambayo si safi na salama.

Wananchi wengi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine  kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.

"" Ni matumaini yangu kwamba ile adha kubwa ya upatikanaji wa  wa maji katika eneo kubwa la kijijini Matumbulu itaisha na kusaidia wanakijiji kupata maji safi na salama kwa wakati"Alisema Mavunde
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Mh Emmanuel Chibago amempongeza Mbunge Mavunde kwa anavyojitoa kuwatumikia wanadodoma na kuwaletea maendeleo na hivyo kuwaomba wanadodoma wampe ushirikiano ili afanye makubwa zaidi.

Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza na wapiga kura wake katika kijiji cha Matumbulu wakati akikabidhi mabomba ya kutandazia maji yenye thamani ya Tsh.8Mill.ikiwa ni moja ni moja ya utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa wakati akiomba kura katikaa ampeni za uchaguzi mkuu 2015







Maoni 1 :

  1. Nakuomba uwe makini na issue ya typing mara kadhaa nasoma humu naona unakosea kuandika tafadhari.

    JibuFuta