Posted by Esta Malibiche on JUNE 12,2018 IN NEWS
Mgeni
rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa
sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika
viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo
12 Juni 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waziri
wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akimkabidhi cheti cha pongezi Mkulima
Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ambaye ameshika
nafasi ya tatu katika msimu wa kilimo cha tumbaku wa mwaka 2017/2018
wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika
katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa
Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Mgeni
rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akikata utepew kuashiria
ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa katika sherehe iliyofanyika
kwenye viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa
Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Waziri
wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akishuhudia
ununuzi wa tumbaku wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku
Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani
Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Baadhi ya wakulima wa tumbaku wakishuhudia sherehe za uzinduzi wa ufunguzi
wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya
Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab Telack akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles
Tizeba wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa
iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama
Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Na Mathias Canal, WK, Kahama-Shinyanga
Waziri
wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amefungua masoko ya tumbaku Kitaifa
huku akitoa onyo kali kwa wakulima waliolima zao hilo nje ya mfumo wa
ushirika kwa mujibu wa sheria ya zao hilo kwa kuwataka kuacha mara moja
kwani serikali itashughulika na wote wanaokiuka taratibu za kilimo
hicho.
Dkt
Tizeba ameyasema hayo leo 12 Juni 2018 katika viwanja vya kata ya
Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati akihutubia mamia
ya wakulima wa tumbaku kwenye sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku
Kitaifa.
Dkt
Tizeba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainabu Telack kufanya
kikao na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya zote za Mkoa huo
kuhakikisha wanazuia wananchi kulima nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu
ya sheria ya zao la tumbaku.
Alisema
kuwa wigo wa soko la tumbaku unazidi kuwa finyu kutokana na viongozi
mbalimbali kuwakumbatia baadhi ya wakulima wa tumbaku wanaolima nje ya
mfumo wa zao hilo.
Katika
sherehe hiyo Mhe Dkt. Tizeba amekabidhi vyeti vya pongezi kwa wakulima
waliofanya vizuri katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 ambao ni
mkulima Emmanuel Cherehani kutoka Wilaya ya Ushetu aliyeshika nafasi ya
kwanza, nafasi ya pili ni Jimson Mwanjwenga kutoka Wilaya ya Chunya
Mkoani Mbeya na Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
Awali
akisoma risala kwa niaba ya wakulima wa zao la tumbaku Tanzania Kaimu
Meneja Mkuu TCJE Ndg Bakari Kisia alisema kuwa zao la tumbaku limeanza
kulimwa nchini Tanzania enzi za ukoloni kwa kuanzia mikoa ya Ruvuma
(Tumbaku ya Moshi) na Iringa (Tumbaku ya mvuke) huku akisema kuwa
umaarufu wa zao hilo umekuja mara baada ya masoko huria kuanzishwa.
Kisia
amepongeza juhudi za serikali katika misimu miwili ya mwaka 2016/2017
na 2017/2018 kwa kutatua suala la kupanda kwa bei ya pembejeo huku
akizitaja changamoto katika zao la tumbaku kuwa ni pamoja na kupungua
kwa mahitaji ya tumbaku, Kushuka kwa bei ya wastani ya tumbaku, pamoja
na Ukubwa wa riba za mikopo.
Akisoma
taarifa ya maendeleo ya zao la tumbaku Tanzania Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Bodi ya tumbaku Tanzania Dkt Julius Ningu ameitaja mikoa inayolima
tumbaku kwa wingi kuwa ni pamoja na Shinyanga, Kagera, Geita, Kigoma,
Tabora, Rukwa, Mbeya, Morogoro, Iringa, Ruvuma na Mara huku akiutaja
mkoa wa Tabora kuongoza kwa uzalishaji kwa takribani asilimia 50 ya
tumbaku yote inayozalishwa nchini.
Alisema
kuwa zao la tumbaku lina mchango mkubwa katika pato la Taifa ambapo
pato la mkulima limeongezeka kutoka shilingi za kitanzania 2,242,030
mwaka 2011/2012 hadi shilingi 5,982,745 mwaka 2016/2017 ambapo ongezeko
hilo ni sawa na asilimia 166.8
Makusanyo
ya ushuru wa Halmashauri za Wilaya yameongezeka kutoka shilingi bilioni
10.8 mwaka 2011/2012 hadi shilingi bilioni 14.8 mwaka 2016/2017
ongezeko la asilimia 37. Huku mapato ya fedha za kigeni yakiwa
yameongezeka kutoka dola milioni 302.8 mwaka 2011 hadi dola milioni
343.9 mwaka 2016/2017 ongezeko la asilimia 14.
MWISHO.
0 maoni:
Chapisha Maoni