Jumamosi, 23 Juni 2018

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI 6 YENYE THAMANI YA BILL.2 WILAYANI NACHINGWEA MKOANI LINDI

Posted by Esta Malibiche on JUNE 23,2018 IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango akikabidhiwa  Mwenge wa Uhuru kutoka kwa  Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi  Joseph Mkirikiti.Makabidhiano hayo yalifanyika jana asubuhi katika kijiji cha Mpiruka mpakani mwa Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea.

Akizungumza na mtandao huu wa habari[KALI YA HABARI BLOG] Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango alisema kuwa jumla ya miradi 6 yenye thamani ya bill.2  imezinduliwa,kukaguliwa na kuwekewa jiwe la msingi.
Mara baada ya kuhitimisha mbio zake wilayani humo,Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa leo wilayani Liwale,ambapo makabidhiano yamefanyika katika kijiji cha Nangano mpakani mwa Nachingwea na Liwale.



Picha ya Pamoja mara baada ya kuzindua mradi wa jengo la shule ya awali na Msingi lililopo kata ya Ugawaji,inayomilikiwa na Masista wa kanisa katoliki Parokia ya Nachingwea.




0 maoni:

Chapisha Maoni