Alhamisi, 7 Juni 2018

SERIKALI YAANZA KUKARABATI CHUO CHA UALIMU NACHINGWEA MKOANI LINDI

Posted by Esta Malibiche on JUNE 8,2018 IN NEWS

Moja ya jengo la Chuo cha Ualimu Nachingwea linalofanyiwa ukarabati.


 Jengo la Chuo cha Ualimu Nachingwea ambalo limefanyiwa ukarabati.Jengo hili ni moja ya darasa lililokuwa limechakaa.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Rukia Muwango akipokea taarifa ya ukarabati wa majengo ya Chuo cha Ualimu Nachingwea.



Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Rukia Muwango akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati wa majengo ya Chuo cha Ualimu Nachingwea Mkoani Lindi.


SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi kiasi cha Mill.900 kwa ajili ya kukarabati  Chuo cha Ualimu Nachingwe Mkoani Lindi.

Akizungumza na mtandao huu wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi katika chuo hicho Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango alisema kuwa aliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kukarabati chuo hicho kongwe kwasababu majengo yake yalikuwa hayaridhishi kutokana na kuchakaa.

"Baada ya kufanya ziara katika Chuo cha Ualimu Nachingwea, nimeridhishwa na Ukarabati unaofanywa katika Chuoni hapo,ujenzi unaendelea kwa kasi pia nimeridhishwa hasa na majengo yaliyojengwa yanaendana na thamani ya fedha zilizotolewa.

Zaidi ya shilingi milioni mia tisa  (900,000,000/=) zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya shughuli hii ya ukarabati Mkubwa inayosimamiwa na Mhandisi Mshauri wa Serikali. Asante Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli kwa yote mema unayotufanyia Wananachingwea. 
Hii italeta hamasa ya ufundishaji na ujifunzaji wa wakufunzi na wanachuo na kupendezesha mazingira. 

Dc Rukia aliwataka wanachuo kuitunza miundombinu !ara itakapokamilia ili iweze kudumu na kwa manufaa ya kizazi kijacho na Taifa kwa ujumla.

"Wanachuo wana wajibu wa kutunza miundombinu hii baada ya kukamilika kwa ukarabati huo Mkubwa ambao haujawahi kufanyika tangu chuo hiki kijengwe mwaka 1976." Alisema Rukia.

0 maoni:

Chapisha Maoni