Posted by Esta Malibiche on JUNE 9,2018 IN NEWS
NA OFISA HABARI MBULU
Mkuu
wa wilaya ya ,Mbulu mkoani Manyara bwana Chelestino
Simbalimile Mofuga ameanzisha kampeni ya wananchi wilayani mbulu kuwa na
vyeti vya kuzaliwa,vifo na ndoa.
kampeni
hiyo imezinduliwa katika kata tatu ikiwemo kata ya ayamaami,uhuru na kata ya
imboru.
Mofuga amesema ni vyema kila mwanchi kuwa na cheti cha kuzaliwa ili kuepuka
usumbufu na kutambulika katika eneo lake kwani mwananchi akiwa na cheti cha kuzaliwa
anakuwa salama na akihitaji huduma ni rahisi kuhudumiwa katika eneo lake.
pamoja
na hilo amesema vyeti vya ndoa na vifo ni muhimu sana kwa mwananchi ili
inapotokea mmoja amefariki itamsaidia ailiyebaki katika kusimamia mirathi bila
kuingiliwa na mtu yeyote wa upande mwingine.
katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Mbulu amesema
kwamba wilaya ya Mbulu inakabiliwa na changamoto
ya matumizi ya risti na kuwataka wananchi kutoa nunua bidhaa katika maduka
ambayo hayatoi risti ili kuepuka usumbufu wa kupelekwa kwenye vyombo vya sheria
kwani mwananchi akikamatwa ana bidhaa aliyonunua bila risiti atafikishwa kwenye
vyombo vya sheria.
katika
maeneo hayo aliyoyapitia nakufanya mkutano wa hadhara mkuu wa wilaya amewataka
wananchi kutopika wala kunywa pombe aina ya gongo na pia kutouza pombe kabla ya
saa tisa alasiri.
Kwa
kata ya Uhuru ameagiza wenyeviti wa mitaa kusimamia wananchi wasinywe kabla ya
saa tisa vinginevyo watawajibika wao wenyewe kwani mtaa wa uhuru unasifika sana
kwa unywaji wa pombe badala ya kufanya kazi.
Katika
kata tatu alizoanza nazo tarehe 8.06.2018 ambazo ni kata ya
Ayamaami,uhuru na Imboru kata ya Imboru mahudhurio hayakuwa mazuri na ameagiza
wenyeviti wa mitaa siku ya tarehe
11.06.2018 kufika katika ofisi yake wakiwa na maelezo ya kutosha ya kwanini
wananchi hawajajitokeza.
Pamoja
na maelezo hayo amewataka wenyeviti waende na tozo ya shilingi 5,000/ kwa kila
kichwa kwa wale wote ambao hawahudhuria
kikao chake cha kiserikali yenye lengo la kutoa maagizo muhimu.
Amesema
wananchi wote ambao hawajashiriki mkutano wake wanafikia 1004 na kwa tozo hizo watakazotoa watafikisha
million tano ambayo imepitishwa kupelekwa kwenye shule ya msingi Isale kwa
ajili ya kupeleka maji.
Kauli mbiu
cheti cha kuzaliwa nyumba kwa nyumba
0 maoni:
Chapisha Maoni