Alhamisi, 14 Juni 2018

MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA WATAKIWA KUHAKIKISHA DAMU INAPATIKANA

Posted by Esta Malibiche on JUNE 14,2018 IN NEWS

IMG_9830
MENEJA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA DKT.MAGDALENA LYIMO AKITOA MAELEZO YA UTARATIBU WA KUCHANGIA DAMU KWA MGENI RASMI MHE.UUMY MWALIMU
IMG_9745
WANAFUNZI WA CHUO CHA UUGUZI MIREMBE WAKISUBIRI KUPATA HUDUMA YA KUCHANGIA DAMU KWENYE VIWANJA VYA NYERERE SQUARE JIJINI DODOMA IKIWA NA MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI
IMG_9771
BAADHI WA WANAJESHI WA JKT WAKICHANGIA DAMU KATIKA MAADHIMISHO HAYO
IMG_9794
MMOJA WA MWANAFUNZI WA NGAZI YA UUGUZI AKICHANGIA DAMU
IMG_9820
IMG_9830
MENEJA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA DKT.MAGDALENA LYIMO AKITOA MAELEZO YA UTARATIBU WA KUCHANGIA DAMU KWA MGENI RASMI MHE.UUMY MWALIMU
IMG_9850
WAZIRI WA AFYA,MWAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU AKIANGALIA KADI YA MCHANGIA DAMU AMBAPO ALIITAKA MPANGO WA DAMU SALAMA KUBORESHA KADI HIZO NA KUWA ZA KISASA ZAIDI
IMG_9871
WAZIRI UMMY MWALIMU AKIONGEA NA MMOJA WA AKINA MAMA WALIOFIKA KUCHANGIA DAMU AMBAPO ALISEMA ASILIMIA KUBWA YA WANUFAIKA WA DAMU SALAMA NI AKINA MAMA WAJAWAZITO NA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI
IMG_9915
WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKIONGEA NA KANALI RAMSON MWAISAKA WAKATI ALIPOFIKA KUCHANGIA DAMU
PICHA ZOTE NA WIZARA YA AFYA
………….
NA.WAMJW-DODOMA
WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU AMEUTAKA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KUHAKIKISHA KUWA DAMU YA KUTOSHA   INAPATIKANA KATIKA MIKOA AMBAYO INAFANYA VIZURI KATIKA UKUSANYAJI WA DAMU ,ILI KUCHOCHEA KASI YA UKUSANYAJI WA DAMU KATIKA MIKOA AMBAYO HAIFANYI VIZURI .
WAZIRI UMMY AMESEMA HAYO LEO JIJINI DODOMA KATIKA VIWANJA VYA NYERERE   KATIKA MAAADHIMISHO YA SIKU YA UCHANGIAJI DAMU KIMATAITA ,AMBAYO KITAIFA IMEFANYIKA JIJINI HAPA.
AIDHA, WAZIRI HUYO AMEENDELEA KUSEMA KUWA ILI KUENDANA NA KASI YA RAISI WA AWAMU YA TANO DKT. JOHN MAGUFULI AMEUTAKA PIA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KWA KUSHIRIKIANA NA MIKOA NA HALMASHURI ZA WILAYA PAMOJA NA JESHI LA WANANCHI KUONGEZA KASI YA UKUSANYAJI WA DAMU KUFIKIA CHUPA 375,203 KWA MWAKA HUU 2018, AMBAYO NI SAWA NA ONGEZEKO LA ASILIMIA 72.
WAKATI HUO HUO WAZIRI UMMY MWALIMU AMEONGEZA KUWA SERIKALI  ITABORESHA UPIMAJI NA UHAKIKI NA USALAMA WA DAMU KWA KUNUNUA MASHINE ZA KISASA KUPITIA BOHARI KUU YA DAWA (MSD)  NA KUSIMIKWA KATIKA VITUO VYOTE VYA KANDA ILI KUBORESHA USALAMA WA DAMU HAPA NCHINI.
KWA UPANDE WAKE KAIMU MKUU WA MKOA WA DODOMA AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA BAHI BI ELIZABETH  KITUNDU AMESEMA KUWA LENGO LA MKOA WA DODOMA KWA MWAKA HUU NI KUKUSANYA CHUPA 9,711 AMBAPO HADI KUFIKIA SASA MKOA UMEKUSANYA  CHUPA 8,826 IKIWA NI ASILIMIA 91 YA LENGO LILILOKUSUDIWA .
NAYE MENEJA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA DKT.MAGDALENA LYIMO AMESEMA LENGO LA MAADHIMISHO HAYA NI KUWAENZI WALE WOTE WANAOCHANGIA DAMU  KWA HIARI NA KUHAKIKISHA HUDUMA YA DAMU SALAMA INAPATIKANA KWA AJILI YA WAGONJWA WOTE WANAOHITAJI, HIVYO WANANCHI KUCHANGIA DAMU MARA KWA MARA NA WALE WENYE DAMU ADIMU KUJIUNGA KWENYE VIKUNDI ILI KUWEZA KUPATIKANA WKWA DAMU KWA MAKUNDI ADIMU.
WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI VIONGOZI WA CHAMA CHA WANAWAKE WACHEZA FILAMU WACHANGIA DAMU KWA HIARI VANITA OMARY MWENYEKITI NA HALIMA YAHAYA KATIBU, WAMESISITIZA WANAWAKE KUJITOKEZA KUCHANGIA DAMU KWANI ASILIMIA KUBWA YA WAHANGA WA DAMU SALAMA NI WANAWAKE .
MAADHIMISHO HAYO HUADHIMISHWA TAR 14 MWEZI WA 6 KILA MWAKA NA KAULI MBIU NI KUWA MWOKOZI  WA MAMISHA JIUNGE NA KIKUNDI CHA WACHANGIA DAMU WENYE KUNDI ADIMU LA DAMU

0 maoni:

Chapisha Maoni