Alhamisi, 14 Juni 2018

HALMASHAURI MPYA YA CHALINZE YATOA MILIONI 140 KWA AJILI YA KUVIWEZESHA VIKUNDI 40 VYA WAJASIRIAMALI VIJANA NA WANAWAKE

Posted by Esta Malibiche on JUNE 14,2018 in NEWS

1
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Erica Egela kulia akimkabishi mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 140 iliyotolewa na halmashauri ya Chalinze kwa lengo la kuweza kuvipatia vikundi vya wanawake na vijana wajasiriamali ,kushoto kwani ni mmoja wa kiongozi wa kundi Emmanuel Tanganyika akikabidhiwa hundi hiyo.(
2
Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Wilayni Bagamoyo Said Zikatimu akizungumza na baadhi ya vikundi vya wajasiriamali kutoka kata ya Msata ambao hawapo pichani waliofika katika halfa yakukabidhiwa hundi hiyo.
3
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Erica Egela akiwahutubia wajasiriamali wa kata ya  Mkata katika halfa hiyo,
4
Mkuu wa idara ya ustawi wa jamii katika halmashauri ya Chalinze Said Mwaipugi akisoma taarifa ya utekelezaji wa utoaji wa mikopo katika halfa hiyo.
PICHA NA VICTOR MASANGU
……………….
NA VICTOR  MASANGU, CHALINZE  
HALMASHAURI mpya ya chalinze iliyopo  Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani katika kuunga mkono  juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika katika kukuza uchumi wa nchi imeamua kuviwezeja kiasi cha shilingi milioni 140 vikundi  vipatavyo  39 vya vijana na wanawake wajasiriamali  kwa lengo la kuweza kukabiliana na wimbi la umasikini na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo.
Hayo yalibainishwa  na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Said Zikatimu wakati wa halfa ya ugawaji wa hundi kwa ajili ya kuvipatia vikundi hivyo vya ujasiriamali kwa vijana na wanawake ambayo imefanyika katika viwanja vya ofisi ya serikali ya mtaa wa Msata  na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali na mashirika binafsi.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba kuwa fedha hizo ambazo zimetolewa zimetokana na makusanyo yatokanayo na mapato ya ndani na kuongeza kuwa halmashauri yake imetenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya   wajasiriamali  kwa lengo la kuweza kuwasaidia kukuza mitaji yao na kujikwamua  kiuchumi.
“Lengo letu kubwa ni kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikishwa kwamba tunawawezesha vijana na wanawake mikopo ya fedha kwa ajili ya kuweza kukuendeleza mitaji yao katika suala zima la shughuli zao za ujasiriamali, na pia kuwajengea uwezo wa kutoa mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia kazi zao la kujipatia kipato,”alisema Zikatimu.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii katika halmashauri ya Chalinze Said Mwakapugi  akisoma taarifa ya utekelezaji wa kuhusiana na utoaji wa mikopo ambapo   vikund I148 vya wanawake na vijana  kutoka kata zipatazo 15 tayari zimeshanufaika na mikopo hiyo ambayo imetokana kupitia asilimia kumi ya fedha za zitokanazo na halmashauri.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Erica Egela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hizo za makabidhiano ya hundi alivitaka vikundi hivyo kuhakikisha wanaitumia vizuri mikopo waliyoipata pamoja na kuwa na mikakati ya kuanzisha  viwanda vido vidogo ambayo vitaweza kuwakomboa kiuchumi.
Nao baadhi ya vijana na wanawake walionufaika na mkopo huo  akiwemo Emmanuel Tanganyika pamoja na Neema Tamla  ambaye ni mjane walisema kuwa fedha hizo wanazopatiwa zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa na  kuwasaidia katika kijikimu kimaisha  na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia shughuli mbali mbali ambazo wanazozifanya.
        
HALMASHAURI mpya ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani mpaka sasa imeshaweza kutoa mikopo kwa vikundi vipatavyo 148 kutoka kata 15 kwa vikundi mbali mbali vua wajasiriamali wanawake pamoja na vijana yenye thamani ya kiasi cha zaidi ya milioni 234 katika bajeti yake ya mwaka  2017-2018.

0 maoni:

Chapisha Maoni