Posted by Esta Malibiche on JUNE 12,2018 IN NEWS
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana
na Ajira Mh Anthony Peter Mavunde amewataka Wazazi na Jamii kutowafanya
Watoto kama chanzo cha mapato kupitia Ajira na kubainisha kwamba
Serikali haitasita kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuwatumikisha
watoto chini ya umri wa miaka 14.
“Watoto
wana haki zao za kimsingi ambazo zinapaswa kulindwa na kamwe wasitumike
kama mgongo wa kuingiza mapato.Watoto waache waishi na kutimiza ndoto
za maisha yao kupitia Elimu na sio kutumikishwa kwa lengo la kupata
ujira”Alisema Mavunde.
Mavunde
ameyasema hayo leo Jijini Mwanza katika kilele cha maadhimisho ya *SIKU
YA KUPINGA AJIRA KWA WATOTO DUNIANI* ambapo ametumia fursa hiyo pia
kuwataka wadau wa masuala ya Watoto kushirikiana na Serikali katika
kutoa ELIMU kwa Jamii ili kutokomeza Ajira kwa watoto ifikapo Mwaka
2025.
Akitoa
maelezo ya awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya *WOTESAWA* Bi Angela
Benedicto ameiomba Serikali kuzifanyia marekebisho sheria
mbalimbali zinazomhusu mtoto ili kuondoa mkanganyiko katika utekelezaji wake.
Jumanne, 12 Juni 2018
NAIBU WAZIRI ANTHONY MAVUNDE AWATAKA WAZAZI KUTOTUMIA AJIRA KWA WATOTO KAMA CHANZO CHA KUJIINGIZIA KIPATO
06:47
No comments
0 maoni:
Chapisha Maoni