Posted by Esta Malibiche on JUNE 7,2018 IN SIASA
|
Mwenyekiti wa chama chama cha
Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akizungumza na Wajumbe[Hapo pichani] wa
Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi.Kulia kwake ni Katibu
wa CCM Mkoa wa Iringa Christopher Magala,kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Mufindi Daudi Yasini.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
MWENYEKTITI wa Chama cha Mapinduzi ccm Mkoa
wa Iringa Albert Chalamila amewataka wajumbe wa Halmashauri kuu ccm wilaya ya
Mufindi kuhakikisha wanafanya ziara
katika maeneo yao ili kutambua changamoto zinazowakabili wananchi ususani
wanachama na kuzipatia ufumbuzi.
Akizungumza leo na wajumbe wa Halmashauri kuu CCM Wilaya ya
Mufindi Mkoani hapa, aliwasihi wajumbe kuendeleza utamaduni wa kuwatembelea
wananchi ili kuibua kero zinazowakabili na kuzifanyia kazi kwa mujibu wa
matakwa ya Irani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.
Chalamila
aliwataka kuzitendea haki dhamana za
uongozi walizonazo katika medali za kisiasa ili
kuhakikisha CCM inazidi kuwa
Chama bora na imara.Pia alitumia fursa hiyo kuvunja rasmi makundi yaliyopo
ambayo yalitokana uchaguzi wa ndani ya chama na jumuiya zake.
Alisema kuwa kumekuwa na mifano mingi ya kukosa majimbo na kata kutokana na kuwa na
makundi ndani ya chama na jumuiya zakE,hivyo kwa uongozi wake hatakubali kuona
majimbo na kata zinachukuliwa na upinzani kutokana na makundi au uzembe wa
kiongozi Fulani.
"Nachukua fursa hii kuvunja makundi yote
ambayo yalikuwepo katika uchaguzi
uliopita ndani ya chama, sisi sote tu wamoja na tunaunganishwa na itikadi ya
chama cha mapinduzi tunapaswa kuungana kukijenga chama chenye sera , taratibu
na misingi ya maadili.Alisema Chalamila
Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe hao,kuhakikisha wanaweka mikakati ya ushindi katika uchaguzi ujao wa serikali
za mitaa na uchaguzi mkuu wa kuhakikisha wanazirudisha ndani ya ccm kata 2
zilizochukuliwa na Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wilayani humo.
Aidha alikemea tabia ya baadhi ya wajumbe
kuingilia utendaji wa wabunge na madiwani,ambappo aliwatakaa waache wabunge wafanye
kazi kwa uhuru mpaka watakapomaliza kipindi chao cha uongozi.
‘Ninawaomba
tuwache wabunge wafanye kazi kwa
uhuru.Kuna wajumbe mmeanza kuwatembeza wagombea wapya majimboni kabla ya muda wake,kwa
kufanya hivyo mnawafanya wabunge washindwe kutatua changamoto zinazowakanbili wananchi.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti Albert Chalamila aliambatana na Mjumbe wa Halamshauri kuu ccm Tanzania bara Tresia Mtewele pamoja na Sekretarieti ya ccm Mkoa
|
|
Mwenyekiti wa chama chama cha
Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akizungumza na Wajumbe[Hapo pichani] wa
Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi.Kulia kwake ni Katibu
wa CCM Mkoa wa Iringa Christopher Magala,kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Mufindi Daudi Yasini.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
|
|
Katibu wa chama chama cha
Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Christophea Magala akizungumza na Wajumbe[Hapo pichani] wa
Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi.Kulia kwake ni makamu Katibu
wa CCM Mkoa wa Iringa,ambae mhasibu kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Albert Chalamila .PICHA NA ESTAMALIBICHE. |
| | | |
|
Katibu wa chama cha mapinduzi ccm Wilaya ya Mufindi akizungumza
|
|
Wajumbe wa Halmashauri kuu CCM Wilaya ya Mufindi wakiwa kat katika kiao. | |
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akikabidhi Tisheti zilizotolewa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ccm Taifa ambae pia ni Mnec wa Mkoa wa Iringa Salim Asas,
Jumla ya tisheti 3600 zimekabidhiwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni