CHAMA cha
Mapinduzi ccm Mkoani Iringa kimetahadharisha kuwafuta uanachama, wanachama wake watakaobainika kuanza kujipitisha kwenye
majimbo na kata kwa lengo la kuomba uongozi huku wabunge na madiwani wa maeneo
yao wakiwa madarakani.
Hayo
yamesemwa jana na Mwenyekiti cha chama cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Albert
Chalamila wakati akizungumza na wajumbe wa Halamshauri kuu ccm Wilaya ya
Iringa vijijini,katika ziara yake ya kwanza toka kuchaguliwa kwake.
Katika ziara
hiyo aliambatana na mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa viti 15 Tanzania bara Teresia
Mtewele pamoja na Sekretarieti ya Mkoa.
Baada ya kukutana na halmashauri kuu ya CCM ya wilaya ya Iringa,Chalamila anatarajia kukutana na wajumbe wa Halamshauri kuu ccm wilaya ya Iringa Mjini hapo kesho.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi ccm Wilaya ya Iringa akizungumza na wajumnbe wa Halmashauri kuu ccm Wilya ya Iringa. Baada ya kukutana na halmashauri kuu ya CCM ya wilaya ya Iringa,Chalamila anatarajia kukutana na wajumbe wa Halamshauri kuu ccm wilaya ya Iringa Mjini hapo kesho.
Makamu katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Bi.Agnes Kasela,akiwasalimia wajumbe wa Halmashauri kuu ccm Wilaya ya Iringa .
Awali Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akivalishwa skafu mapema leo asubuhi mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Iringa mjini tayari kuanza ziara yake wilayani humo.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Iringa,akiwa na katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa James Mgego.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa Dodo Sambu akiwa na Katibu Mwenezi CCM wilaya ya Iringa.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ccm Wilaya ya Iringa wakimsikiliza Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Albert Chalamila.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ccm Wilaya ya Iringa wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa Christopher Magala.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ccm Wilaya ya Iringa,wakiwa kwenye kikao. |
0 maoni:
Chapisha Maoni