WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watu wenye ulemavu ndani na badala yake kuwaibua ili waweze kupata haki zao za msingi.
Hayo yamesemwa leo na askofu wa jimbo katoliki la Njombe Alfredy Maluma wakati akitoa homilia yake katika ibada ya misa takatifu ya mazishi ya kuwaaga na kuwaombea Marehemu mapacha walioungana Maria na Consolata iliyofanyika katika viwanja vya Chuo kikuu cha Katoliki Ruaha Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ya seriakali akiwemo waziri wa Elimu Joyce Ndalichako,naibu waziri anayeshugulikiwa walemavu Stela Ikupa,wawakilishi wa wabunge ,wabunge wa mkoa wa Iringa,wakuu wa wilaya wa mkoa wa njombe,viongoze wa vyama vya siasa,viongozi wa dini.
Akizungumza alisema Taifa linapaswa kuwapenda na kuwathamani watu wenye ulemavu kama ambavyo shirika la Bikira Maria wa Consolata lilivyojito kuwasaidia walemavu hao katikakipindi chote cha Uhai wao.
Askofu Alfredy alisema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la wananachi kuwanyanyasa watu wenye ulemavu na wengine kuwaona mizigo hali inayopelekea watu wenye ulemavu kukosa huduma muhimu wanazostahili kupata.
Kila binadamu hapa duniani kaumbwa kwa sura na Mfano wa Mungu,hivyo inatupasa tutafakari juu ya wajibu wetu kuhusu uhai ,tukidhaminiana na na kupendana kwa dhati bila kubaguana.

Nae waziri wa elimu,sayansi na teknolijia Profesa Joyce Ndalichako akitoa salamu kwa niaba ya serikali alisema kuwa watanzania wanapaswa kuiga maisha ya Maria na Consolata kutokana na ushujaa wao wa kupambana kuweka bidii katika masomo yao.
Watanzania tunatakiwa tujifunze kupitia maisha ikiwa nipamoja na kujenga utamaduni wa kuvumiliana,kupendana na kushirikiana kuhu tukitafakari kujiepusha mifarakano katika kazi,familia na jamii kwa ujumla.
‘Serikal hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli inawapenda watanzania wote na imeweka kipumbele kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata Elimu kuanzia msingi mpaka chuo,pia serikali kwa kuwathamini watu wenye ulemavu imeweza kufanya teuzi na tunaona mawaziri na mabalozi ambao ni watu wenye ulemavu.
Ndalichako alisema kuwa jamii inatakiwa kuachana na dhana potofu ya kumficha mtoto mwenye ulemavu ndani,na kusema kuwa ulemavu ni maumbile tu wanapaswa kupata huduma muhimu kama wengine.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni