Jumatano, 6 Juni 2018

DC MBULU ASHUSHA BEI YA NYAMA

Posted by Esta Malibiche On  JUNE 6,2018 IN NEWS

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara bwana Chelestino Mofuga  amekutana na wafanyabiashara  wa nyama ili kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza kati yao na wananchi.
Kikao hicho kilifanyika katika  ukumbi wa community center katika  Halmashauri ya mji wa Mbulu tarehe 06.06.2018.
Mkuu wa wilaya bwana  Mofuga mwanzo wa kikao aliwataka wafanyabiashara hao watoe sababu zinazofanya bei ya nyama Mbulu iwe  juu kuliko sehemu nyingine.
Baadhi ya wafanyabiashara Philipo Shauri alisema nyama bei  iko juu kwa sababu Ng'ombe kwa wilaya ya Mbulu hawapatikani kama ilivyodhaniwa na wengi.
Wakati wa mvutano huo wafanyabiashara hao hawakuonyesha utayari wa kupunguza bei  hiyo kutoka 7000/ baada ya Mkuu wa wilaya kuonyesha msimamo wake bei  ilipendekezwa kuwa iwe  6000/ kwa kg moja.
Wafanyabiashara hao wakaomba wiki moja kabla ya kushusha bei  ili wajiandae kwa mabadiliko mpya ya bei  na Mkuu wa Wilaya akawapa siku  saba kutoka tarehe 6.6.2018 hadi  13.06.2018.
Bwana Mofuga  amehitimisha kwa kuwataka wafanyabiashara hao kutii makubaliano hayo yaliyoafikiwa na pande zote mbili.




0 maoni:

Chapisha Maoni