Ijumaa, 8 Juni 2018

DC MOFUGA:WAFANYABIASHARA HAKIKISHENI MNATOA RISITI KWA WATEJA WENU.

Posted by Esta Malibiche on JUNE 9,2018 IN NEWS
NA OFISA HABARI MBULU


Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara amewataka wafanyabiashara wilayni humo  kutoa risiti baada ya kuuza bidhaa.


Mkuu wa Wilaya bwana Chelestino Mofuga amesema hayo katika  kikao cha pamoja na wafanyabiashara walioitikia wito  wake katika  ukumbi wa community center siku  ya tarehe 5.6.2018 .


Kikao hicho kimewashirikisha Meneja wa TRA Mbulu na afisa biashara wa Halmashauri ya mji wa Mbulu.

 Bwana Mofuga amesema kila atakaye kiuka masharti ya serikali anavunja Sheria kwani ni  lazima Mwananchi akinunua bidhaa apewe risiti na kama hajapewa adai risiti.


Aidha amesema kwa wafanyabiashara wote  wenye vigezo vya kutumia machine za EFD ni  lazima watumie mashine  ili kuepuka usumbufu kwenye biashara zao.


Kwa wale ambao ni  wafanyabiashara wadogo watumie risiti za kuandika kwa mkono kwa lengo la  usalama wa biashara zao.


Katika  hatua nyingine Amewataka wamiliki wa Magari kununua Magari mapya wakati huu ambapo serikali inafanya marebekebisho makubwa ya ujenzi wa barabara ya lami kama ilivyo kwenye ilani ya CCM 2015-2020.



Amehitimisha kwa kusema ukiuza toa  risiti na ukinunua dai risiti. Na kodi ni kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania.

0 maoni:

Chapisha Maoni