Jumamosi, 3 Machi 2018

WAZIRI NDALICHAKO ATOA MIEZI MITATU KWA MAOFISA ELIMU NCHINI

Posted by Esta Malibiche on March 3,2018 IN NEWS





Serikali imetoa miezi mitatu kwa Maofisa elimu wa mikoa kuhakikisha wanaondoa mlundikano wa wanafunzi madarasani hasa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu 2018

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalicha alipokuwa akifunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara, mjini hapa.

"Wamefanya vibaya katika uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza na kusababisha darasa moja kuwa na wanafunzi zaidi y
a elimu anayefuata miongozo yetu inayotaka darasa moja kuwa na wanafunzi 40, na unajua miundombinu ilivyo inakuwaje unafanya uchaguzi watoto 200 wanaenda kukaa darasa moja."Alisema Ndalichako na kuongeza kuwa 

 Nina taarifa za baadhi ya wanafunzi wa sekondari wanasomea nje, nikasema siendi huko kwani hilo ni kosa la kiholela, nawapa miezi mitatu mkashughulikie hili,” alisema.

Alisema kuwa kwa watakaoshindwa kushughulikia tatizo la mlundikano wa wanafunzi, atapeleka majina yao kwa Waziri wa Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ili awachukulie hatua.


 Profesa Ndalichako alisema uchaguzi wa wanafunzi unategemea nafasi na miundombinu iliyopita na si kwa kila aliyefaulu achaguliwe na kusisitiza mlundikano ndani ya darasa haukubaliki.Aidha, aliagiza shule zote za kidato cha tano ambazo hazijasajiliwa zikaguliwe na zilizokidhi viwango zisajiliwe ili zipokee wanafunzi wa kidato cha tano.

Alihitimisha kwa kusema  kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili maofisa hao ikiwemo suala la usafiri na kwamba katika kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi kwenye taaluma, serikali imeagiza pikipiki 2,800 kwa ajili ya waratibu elimu kata. Awali, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tamisemi (ELIMU), Tixon Nzunda alisema katika kikao maofisa hao wameahdi kufuta ziro kwenye shule za umma

0 maoni:

Chapisha Maoni