Alhamisi, 22 Machi 2018

MWENYEKITI WA UWT TAIFA GAUDENSIA KABAKA AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA

Posted by Esta Malibiche on March 22,2018 in SIASA

  Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akizungumza na wananachi wa Idodi alipowatembelea jana ikiwa ni moja ya ziara yale ya kukagua  upanuzi wa kituo cha Afya Idodi.


Na Esta Malibiche

Iringa

Wananchi wa kijiji cha Idodi kata ya Idodi Tarafa ya Tungamalenga wameishukuru Serikali ya awamau ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongezwa na Dakta John Magufuli kwa  kuwapatia kiasi cha fedha  kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha Afya Idodi.

Akisoma Taarifa  ya upanuzi wa kituo hicho kwa Mwenyekiti wa UWT  Taifa Bi.Gaudansia Kabaka, Diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo alisema kuwa Serikali imewawezesha kwa kutoa kiasi cha Mill 400,huku ikishirikiana na Benki kuu ya Dunia pamoja na  Seriakali ya Denmark.

 Mtatifikolo alisema kuwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na    wameweza kuchangia  kiasi cha  Mill.400 ambazo zitasaidia kukamilisha majengo hayo ambayo yanatarajiwa kukamilika mapema na kukabidhiwa April 30,2018
Alisema kuwa  majengo yanayoongezwa ni wodi ya akina mama,chumba cha Upasuaji mkubwa,Maabara,Jengo la kuhifadhia maiti pamoja na Nyumba ya moja ya mtumishi ambapo mpaka kukamilika kwake itagharimu kiasi cha Tsh.396,861.56.


 Aliongeza kuwa ili kuunganisha majengo yaliyopo na majengo mapya  wanahitaji ujenzi wa  corido za nje zitakazotumika kusafirisha wagonjwa  kutika jengo moja  kwenda jengo jingine.

  Aliongeza kuwa muonekano wa majengo yaliyopo na miundombinu yake ni chakavu ,hivyo kinahitaji kiasi cha fedha  kisichopungua Tsh.30,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya zamani na miundombinu yake.

Kwa upande wake katibu wa UWT kata ya Idodi  Elizabeth Kiseo akisoma Taarifa ya Umoja wa Wanawake Tanzania  kata ya Idodi  kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa alisema kuwa pamoja na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali wanazofanyab kupitia vikundi vyao vya VICOBA,wameiomba Halmashauri ya kiji cha Idodi shamba kwa ajili ya kupanda miche ya Korosho ili kuendana na kasi ya Uchumi.

‘Ndugu Mwenyekiti pamoja na kupata mikopo katika Halmashauri yetu, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadau wanaoviwezesha vikundi vyetu hasa Mbunge wa Jimbo la Isimani Mh.Willium Lukuvi,Diwani wa akata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo, amadiwani wa viti maalum,Halmashauri ya wilaya ya Iringa pamoja na aviongozi mbalimbali wa Serikali’Alisema Kiseo’

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akijibu tarifa hiyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo kupitria chama cha Mapinduzi CCM Willium Lukuvi kwa juhudi za kukahikisha wananachi wake wanapata huduma muhimu ikiwemo Afya.

Kabaka aliwasihi wananchi kuhakikisha wanashirkiana na Serikali ili ujenzi unaoendelea wa kupanua kituo cha Afya uweze kukamilika kwa wakati,hivyo waweze kuondokana na adha wanayoipata.

‘Kwa uchungu mnaoupata kutokana na kituo hiki kukosa huduma muhimu  kama mlivyosema katika taarifa yenu,ninawaomba mjitoe pale mnapohitajika.Kituo hiki kikikamilika hamtakuwa na sababau ya kwenda kupata matibabau katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,na hivyo kupoteza muda na kutembea umbali mrefu’’Alisema Kabaka.
Aidha aliwataka wanawake kuchangamkia Fursa zinazotolewa na Serikali kwa kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili wawaeze kunufaika na mikopo inayotolewa  katika benki mbalimbali zilizopo  hapa Nchini.

'Wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa maendeleo yako.''Alisema Kabaka



Katibu wa Chama cha Mpainduzi CCM  Mkoa wa  Iringa Christopher Magala akizungumza na wananachi wa Idodi

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa Nikolina Lulandala akizungumza na wananchi wa Idodi
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Iringa Vijijini akizungumza na wananchi wa Idodi

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Iringa Vijijini akizungumza na wananchi wa Idodi





  Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Idodi.
 Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Idodi.
 Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akishiriki ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Idodi.
 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa Nikolina Lulandala  akishiriki ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Idodi.
 
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iringa Vijiji akishiriki ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Idodi

Moja ya jengo linaloongezwa katika Kituo cha Afya Idodi
 Ujenzi ukiendelea katika  Majengo yanayoongezwa katika Kituo cha Afya Idodi
Ujenzi ukiendelea katika  Majengo yanayoongezwa katika Kituo cha Afya Idodi
 Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akipanda mti katika Eneo la UWT Mkoa lililopo katika kijiji cha Tungamalenga kata ya Idodi Tarafa ya Idodi
 Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akiendelea kufukia  mti katika  Eneo la UWT Mkoa lililopo katika kijiji cha Tungamalenga kata ya Idodi Tarafa ya Idodi
 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa Bi.Nikolina Lulandala akipanda mtikatika  Eneo la UWT Mkoa lililopo katika kijiji cha Tungamalenga kata ya Idodi Tarafa ya Idodi




0 maoni:

Chapisha Maoni