Ijumaa, 23 Machi 2018

MWENYEKITI WA UWT TAIFA GAUDENSIA KABAKA AWATAKA WANAWAKE KUTUMIA MAALIFA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Posted by Esta Malibiche on March 24,2018 in SIASA
Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akizungumza na UWT tarafa ya Pawaga,Halmshauri ya Iringa Vijijini,katika ziara yake aliyoifanya Mkoani Iringa huku akiambatana na viongozi Mbalimbali wa UWT Taifa.



Na Esta Malibiche
Iringa

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa chama cha  ccm Taifa UWT  Bi.Gaudensia Kabaka amewataka wanawake kuacha kubweteka bali wafanye kazi kwa bidii ikiwa nipamoja na skujishughulisha katika biashara ndogondogo  ili wawaeze kujikwamua katika wimbi la kuwa tegemezi.


Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na UWT Tarafa ya Pawaga wakati wa ziara yake aliyoifanya Mkoani Iringa,kwa  lengo la kukagua shughuli za Maendeleo zinazofanywa na UWT pamoja na kupokea changamoto zinazowakabili wanawake Mkoani hapa.

'Wanawake tunatakiwa tujiajili,tufanye kazi ikiwemo kilimo ambacho hakimtupi mkulima ili tuweze kujikwamua kiuchumi'Alisema kabaka.

 Kabaka  alisema kuwa muda wa kukaa na kusubiri kupewa umeisha,hivyo wanawake wanatakiwa kuamka na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuendana na kasi ya Mh.Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Magufuli ya Hapa Kazi tu.

Aidha aliwataka vijana kuacha kutumika na wanasiasa ambao hawalitakii mema Taifa letu,ambao wanawashawishi kuivuruga Amani iliypo Nchini kwa maslai yao binafsi.

'Kijana mzalendo ni yule anaeipenda nchi yake na kuitumikia nasi yule anaechochea vurugu na kuhatarisha Amani ya Nchi yake  kwa maandamano,hivyo vijana acheni kutumika na wanasiasa wasioitakia mema Nchi yetu.'Alisema Kabaka

Vijana mlioko vyuoni someni kwa bidii Taifa linawategemea na kwa wale ambao hamko masomeni fanyeni kazi ikiwemo kilimo ili muweze kujikwamua kiuchumi''Alisema Kabaka.

Hata hivyo aliwasihi wazazi kupanga muda wa kuzungumza na wataoto wao hasa vijana ili wasiweze kujiingiza katika matukio yasiyofaa katika jamii na Taifa kwa ujumla.

 Kwa upande wake Katibu wa UWT kata ya Idodi Agnes Kayagwa,Akisoma taarifa ya maendeleo ya UWT tarafa ya pawaga kwa  Mwekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka,  alisema kuwa Katika kutekeleza sera ya viwanda Nchini ,tarafa ya pawaga iliyopo Halmashauri ya Iringa Vijijini imeendele imeunga mkono sera hiyo kwa kuunda na kupata ambayo imewawezesha  kumiliki vifaa vya kilimo kama pawatila kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Kayagwa kutokana na Serikali ya awamu ya Tano kuelekeza kila Mkoa uhakikishea unakuwa na viwanda 100 ili kuendana na Tanzania ya Viwanda,UWT Pawaga  walilipokea kwa mikono miwili na kuanza kutekeleza kwa vitendo kwa kujiunga katika vyama vya ushirika vinavyomiliki mashine za kukoboa mpunga na kufuangua viwanda vidogovidogo vya ushonaji.

Mh.Mwenyekiti,Tarafa ya Pawaga ina jumla ya vikundi 104 kati ya hivyo vikundi vya wanawake ni 82 Vicoba 8 na mchanganyiko 16.hivyo,katika kujikwamua kiuchumi kwa mwaka 2017/2018 kimetumia kiasi cha  Tsh.19,000.000 kimetumika kukopesha vikundi vya wanawake,ambapo jumla ya vikundi 19 vimepokea mkopo kutoka mfuko wa wanawake wa Halmashauri ya wilaya kwa ajili ya shughuli za Kilimo na Biashara’Alisema Kayagwa.

Kayagwa alisema  kuwa wanaiunga mkono serikali kwa kupiga vita  maadui watatu ambao ni Umasikini,Ujinga na Maradhi wanawake wa Tarafa ya Pawaga wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia Shughuli za Maendeleo,ambapo mpaka sasa jumla ya miradi 15 ya maendeleo imetekelezwa  katika sekta ya Afya,Elimu na  Kilimo ambapo wananchi wameshiriki kujenga vyumba vya madarasa,Mabweni ,Maabara,nyumba za Walimu,Zahanati na Maghara ya kuhifadhia Chakula na Mazao ya Biashara.

Akizungumzia mafanikio alisema kuwa kwa kushirikiana na  serikali hii ya awamu ya Tano  wameweza kufanikiwa kupata mradi mkubwa wa uboreshaji wa maji bomba kwa lengo la kumtua mwanamke ndoo ichwani,ambao umegharimu kiasi cha Tsh.5.Bill.ambapo hadi sasa mkandarasi ameshapatikana.

‘Tunaishukuru Serikali kwa kutupunguzia michango mashuleni kutokana na  sera ya Elimu bila Malipo.Pia imeboresha baadhi ya miundombinu ya umwagiliaji katika skimu ya kilima,magozi na Mlinge.

 Hata hivyo aliiomba Serikali kupitia wizara ya Maliasili na utalii isaidie kufungua lango la kungilia hifadhi ya Taifa Ruaha ili wawaze kunufaika na Fursa zinazotokana na watalii wanaoingia na kutoka katika Hifadhi kupitia Pawaga.
Mwenyekiti wa  UWT Taifa Bi. Gaudensia Kabaka amewataka wanawake kujitegemea kwa kujishughulisha na  ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mashine ya kisasa ya kukoboa Mpunga inayomilikiwa na vyama vya Ushirika Tarafa ya Pawaga .

 Ghara la kuhifadhia mazao
 
 Jengo la ghara la kuhifadhia Mazao



 Mwenyekiti wa UWT Taifa akipata maelekezo kutoka kwa Diwani namna wanavyotumia vifungashio kwa ajili ya kuhifadhia Mchele Unapokobolewa

 Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akikagua kazi za mikono zinazofanywa na akina mama wa UWT Tarafa ya Pawaga wanaojihusisha na ushonaji.
 
  Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akizungumza na  akina mama wa UWT Tarafa ya Pawaga wanaojihusisha na ushonaji alipowatembelea kukagua shughul i za maendeleo







 Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Gaudensia Kabaka akizungumza na UWT tarafa ya Pawaga,Halmshauri ya Iringa Vijijini,katika ziara yake aliyoifanya Mkoani Iringa huku akiambatana na viongozi Mbalimbali wa UWT Taifa.
 


 Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Christopher Magala akizungumza na wananachi wa Tarafa ya Pawaga katika ziara ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Mkoani Iringa.
 
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Irina Bi.Nikolina Lulandala akizungumza na wananachi wa Tarafa ya Pawaga
 
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Costantino Kihwele alkizungumza na wananachi wa Tarafa ya Pawaga

Katibu wa Chama Cha Mpinduzi CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Dodo Sambu akizungumza na wananachi wa Tarafa ya Pawaga
 
 Makamu  Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya  Ritha Mlangala akizungumza na wananachi wa Tarafa ya Pawaga
 Katibu wa UWT Wilaya ya Iringa Vijijini Bi.Asha Stambuli akizungumza na wananachi wa Tarafa ya Pawaga

Katibu wa Jumuiya ya Vijana UVCCM Mkoa wa Iringa James Mgego akizungumza
Katibu wa UWT.Tarafa ya Pawaga Bi. Agnes Kayogwa akisoma  taarifa ya maendeleo ya UWT Tarafa ya Pawaga kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa.





















Wanachama  wapya 50 waliojiunga na UWT  katika Tarafa ya Pawaga wakati wa ziara ya Mwenyekiti  wa UWT alipowatembelea.



Shammba la Mpunga











0 maoni:

Chapisha Maoni