Alhamisi, 1 Machi 2018

MAMA SAMIA AWATAKA SKAUTI NCHINI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI KUJIONGEZEA KIPATO*

Posted by Esta Malibiche ON March 2,218 IN NEWS


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan amewataka Skauti nchini Tanzania kushiriki katika shughuli za Uzalishaji mali kwa lengo la kujiongezea kipato na kukabiliana na changamoto ya Ukosefu wa Ajira hasa kwa Vijana.

Hayo yamesemwa leo Mkoani Dodoma katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Skauti Nchini uliofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa ambapo Hotuba ya Makamu wa Rais ilisomwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Mavunde* ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Mdhamini wa Skauti Tanzania,Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mh Ali Hassan Mwinyi.

Aidha akimkaribisha Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Skauti Tanzania Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry amebainisha mipango mbalimbali ya Skauti Tanzania katika kujiletea maendeleo na pia amemhakikishia Mgeni Rasmi kwamba Skauti Tanzania itaendelea kujikita katika kusimamia *HAKI,USAWA* na *UZALENDO* pamoja na kuhimiza *AMANI* na *MSHIKAMANO* miongoni mwa Watanzania.

Mkutano huu Mkuu wa Skauti agenda yake kuu ni Uchaguzi wa Uongozi wa Skauti na Wajumbe wa Bodi.Kwasasa sasa Skauti Tanzania ipo chini ya Uongozi wa Skauti Mkuu Mama Mwantumu Mahiza na Kamishna Mkuu Abdulkarim Esmail Shah







0 maoni:

Chapisha Maoni