Posted by Esta Malibiche on March 5,2018 IN SIASA
Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Tanga ndugu Omary Saidi Mwanga ameongoza baraza la vijana mkoa wa Tanga pamoja na mambo mengine baraza hilo limewachagua ndugu Walter Mwai, ndugu Mwanaisha Manofu na ndugu Hamisi Sadiki kuwa wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya mkoa.
Awali, Katibu wa CCM mkoa wa Tanga ndugu *Allan kingazi* amewaasa wajumbe hao wa baraza kuwa na nidhamu, utii na uwajibikaji katika shughuli zao za kila siku. Pia wawe vijana makini kusimamia rasilimali za chama na jumuiya ili ziwe na manufaa zaidi. Akiongezea, amewataka wajumbe hao kukagua miradi inayotekelezwa na serikali ili kuona namna ilani ya chama cha mapinduzi 2015 inavyotekelezwa.
Nae mjumbe wa baraza kuu taifa kutoka mkoa wa tanga ndugu *Lucy mganga* amewasisitiza viongozi wa ngazi ya wilaya na kata kuongeza zaidi wanachama katika maeneo yao lakini pia nidhamu na uwajibikaji katika shughuli zao za kila siku.
Aidha, mwenyekiti uvccm mkoa wa tanga ndugu *Omari Mwanga* aliwahimiza wajumbe hao kusimamia rasilimali za chama kwenye maeneo yao, kufanya ziara katika ngazi ya kata na mitaa ili kuzifahamu na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakumba vijana wenzetu. Pia amewasisitiza wajumbe hao kushiriki katika shughuli za kijamii na za kujipatia kipato ili kujikwamua kimaisha.
Mwisho, Mwenyekiti wa vijana mkoa tanga ndugu *Omari Mwanga* amempongeza mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Dkt. John Pombe Magufuli* kwa utendaji kazi wake anayotukuka wa kazi anayofanya ya kujenga nchi.
Pia alimpongeza mwenyekiti UVCCM Taifa ndugu *Kheri James (MCC)* kwa kazi kubwa anayofanya ya kuimarisha jumuiya ya vijana.
Imetolewa na;
Ofisi ya jumuiya ya vijana (CCM)
Mkoa wa Tanga
Jumatatu, 5 Machi 2018
UVCCM MKOA WA TANGA WAFANYA BARAZA LA VIJANA LA MKOA
11:35
No comments
0 maoni:
Chapisha Maoni