Jumamosi, 10 Machi 2018

JAFO AWATAKA WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

Posted by Esta Malibiche on March 10,2018 IN MICHEZO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa wizara yake.

..........................................................
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo ameongoza zoezi la kufanya mazoezi kwa watumishi wa Wizara hiyo na Taasisi zake za Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mfuko wa Pension wa LAPF, Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa (LGLB), Wakala wa Barabara za Vijijini(TARURA) na Shirika la Elimu Kibaha (KEC) huku akitoa wito kwa Watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi.

Mazoezi hayo yamelenga kujenga afya kwa Watanzania na kujiondoa katika hatari ya magonjwa nyemelezi ambapo michezo ya Soka, Riadha, kutembea kwa kasi na Kuvuta kamba ilishindaniwa.

Mhe. Jafo ameambatana na Viongozi wengine wakiwemo Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda, Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Zainab Chaula, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deogratius Ndejembi na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Dodoma, pia baadhi yakazi wa Manispaa ya Dodoma.

Akizungumza wakati wa mazoezi hayo yaliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri Mkoani hapa, Jafo alisema Watanzania wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuiweka miili yao vizuri na ametoa agizo kwa  ofisi yake kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara moja ili kufahamiana pamoja na kujenga hamasa ya kufanya kazi.

“Haya mazoezi tunamuunga mkono Makamu wa Rais Mama Samia katika juhudi zake za kufanya mazoezi,mazoezi ni muhimu kwa afya sasa kila mwezi tutakuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi  mara moja kwa mwezi ili kuongeza hamasa ya kufanya kazi,”alisema.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda alitoa dua maalum ya kuombea wote waliohudhuria, Mhe. Rais John Magufuli na kumshukuru Mhe. Jafo kwa kuandaa bonanza hilo ambalo linaleta hamasa, upendo na mshikamano wa watumishi Umma na watanzania.

Naye Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Afya, Dk.Zainabu Chaula alimshukuru Jafo kwa kuandaa mazoezi hayo kwani yatawasaidia k kujenga afya pamoja na kupongeza hamasa ya kufanya kazi.

Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Mahenge alisema kutokana na Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi ni lazima kuwe na viwanja bora vya Michezo.

“Mheshimiwa Rais ameanza ujenzi wa Uwanja wa michezo wa Kisasa katika eneo la Nzuguni  lazima tumuunge mkono kwani tunataka Mkoa wa Dodoma uwe wa kuvutia hivyo ni lazima kuwe na viwanja vingi vya michezo.

0 maoni:

Chapisha Maoni