Jumatano, 7 Machi 2018

MAVUNDE AIBUKIA TEMEKE,AAGIZA WAAJIRI ZAIDI KUFIKISHWA MAHAKAMAWATAKA WAAJIRI KUTOA MIKATABA KWA MUJIBU WA SHERIA

Posted by Esta Malibiche ON March 6,2018 IN NEWS

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde leo ameendelea na ziara ya ukaguzi mahala pa Kazi ambapo leo ametembelea Wilaya ya Temeke,Dar es Salaam na kuagiza Waajiri wote ambao hawajajisajili katika mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kufikishwa mahakamani mara moja kwa kukiuka matakwa ya *Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Sura ya 263 ya Mwaka 2008* ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaam jumla ya waajiri *6907* bado hawajajisajili katika mfuko huo.

Mh Mavunde pia amefunga uzalishaji wa kiwanda cha Bhogal Chamanzi,Mbagala kwa kukiuka masharti ya sheria ya *USALAMA* na *AFYA* mahala pa kazi na kuamuru kukamatwa kwa raia watatu wenye asili ya Kihindi kwa kutokuwa na Vibali vya kufanya kazi nchini huku akiagiza mwajiri huyo kutoa mikataba kwa wafanyakazi wake ndani ya siku thelathini(30).

Wakati huo huo Naibu Waziri Mavunde amekitoza faini ya *Tsh 14,250,000* kiwanda cha *Camel Concrete Ltd* kwa kukiuka kwa kiwango kikubwa sana masharti yaliyoainishwa katika *Sheria ya Afya na Usalama mahala pa kazi,Na.5 ya 2003* na kutaka Mwajiri kuhakikisha anatoa mikataba inayokidhi matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/2004.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Kamishna wa Kazi Bi Hilda Kabisa amewatahadharisha waajiri wote ambao watashindwa kufuata matakwa ya Sheria mbalimbali zinazoongoza masuala ya kazi kwamba watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria hizo bila kusita na kuwa mkono wa serikali utawafikia wote.

0 maoni:

Chapisha Maoni