Ijumaa, 2 Machi 2018

MAVUNDE AWASILI MKOANI TANGA LEO HII KUENDELEA NA ZIARA YA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA SHERIA MBALIMBALI ZA KAZI

Posted by Esta Malibiche on March in NEWS
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi CCM  Mh Anthony Peter Mavunde akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela mara baada ya kuwasili Mkoani humo mapema leo hii asubuhi tari kwa kuanza ziara ya kikazi.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Anthony Peter Mavunde leo anaanza ziara katika mkoa wa Tanga kufuatilia utekelezaji wa sheria mbalimbali zinazohusu masuala ya Kazi.

Mavunde alianza ziara yake kwa kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Martin Shigella na baadaye kukutana na Viongozi wa CCM MKOA wa TANGA chini ya katibu wa Mkoa Comrade Allan Kingazi.

Mavunde yupo katika operesheni maalum ya kukagua viwango vya kazi pamoja na kuwabaini Waajiri wote ambao hawajajisajili katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Anthony Peter Mavunde ,ambae pia ni Mbumge wa Ji!bo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM,akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.




Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Anthony Peter Mavunde ambae pia ni Mbumge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitianChama cha Mapinduzi CCM,akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga alipowasili mapemamleo hii tayari kwa kuanza ziara yake ya kikazi Mkoani humo.





0 maoni:

Chapisha Maoni