Posted by Esta Malibiche on March 6,2018 IN NEWS
Shukrani hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,Ridhiwani Kiwete wakati akizungumza na wananchi katika eneo linalojengwa kituo cha Afya na ambapo alishirikiana na wananachi wake katika ujenzi.
Baad ya kupokea vifaa hivyo,Ridhiwani alimpongeza Rais Mstaafu kwa msaada huo na pia kutambua mchango mkubwa alioufanya katika jimbo hilo.
"Tukiwa mkutanoni , tukapata Ujumbe Mzito wa Raisi Mstaafu na Mkulima maarufu akiwa ma Mama Salma (Mb). Ujio wao sio tu ulileta Furaha kwa Wananchi lakini Pia ahadi ya Kuunga mkono juhudi za wanamaendeleo kwa kuchangia Mifuko 300 ya Cementi ilitolewa.Mifuko hii sasa inapelekwa kwa Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji Cha Kwakonje baada ya kupata Madarasa 8 Msaada toka Tanapa na Milioni 250 toka Serikali Kuu kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kibindu"" Alisema Ridhiwaninna kuongeza kuwa
Tunamshukuru Mbunge wa kwanza wa Jimbo laChalinze ambae pia ni Rais Mstaafu Dakta Jakaya Mlisho Kikwete,kwa kuchangia Vifaa h(vi.Pia ninawaomba wadau wengine wa Maendeleo kujitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha jimbo la Chalinze linasonga Mbele kimaendeleo.
Kwa upandewake Mh. Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dakta Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo alisema kuwa lengo la kutoa mifuko hiyo ni kutokana na kuridhishwa na mwenendo mzima wa jimbo hilo kwa sasa na kujionea tofauti wake na wa sasa katika upatikanaji wa huduma za wananchi wa chalinze.
Aidha Dkt Kikwete amempongeza mbunge huyo kwa jitihada anazofanya katika kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo yenye tija na manufaa kwa ajili ya kukuza uchumi wao.
"Wakati nikiwa mbunge kulikuwa hakuna mambo mazuri kama yalivyo sasa hivyo wana chalinze wenzangu nawaombeni tumshike mkono mbunge wetu ili atufikishe salama kule tuendako alisema.
Aliongeza kuwa uongozi mzuri ni ule wa kuacha alama katika Taifa na hili ndilo naliona mnafanya.
Kwa Upande wa Mama SalmaKikwete( Mb) pamoja na kuchangia mifuko ya Saruji naye pia aliwapongeza hasa wakina mama wa Kibindu kwa jinsi wanavyojitoa kwenye shughuli za maendeleo.
0 maoni:
Chapisha Maoni