Jumapili, 4 Machi 2018

PROFUTURO KUMWAGA VISHKWAMBI (TABLETS) VYENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI MOJA KATIKA SHULE ZA DODOMA MJINI

Posted by Esta Malibiche ON March 4,2018 IN   NEWS




 Shirika la PROFUTURO la Hispania ambao ni wadau wakubwa katika sekta ya Elimu Duniani wamekubali kulisaidia Jimbo la Dodoma Mjini kwa kugawa tena Tablets(Vishkwambi) 750 na Laptops zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya Shule za Msingi na Sekondari zilizopo   Jimbo la Dodoma Mjini ambalo lipo chini ya uwakilishi wa Mh Anthony Peter Mavunde.

Leongo la kutoa vifaa hivyo ni  kuunga   mkono jitihada zinazofanywa na Mbunge huyo katika kusaidia sekta ya Elimu Jimboni kwake, lakini pia kutokana na Shule za Dodoma Mjini kufanya vizuri katika matumizi ya Vishkwambi 500 vilivyotolewa mwaka jana 2017.

Mwaka 2017 Shirika la PROFUTUROlilisaidia Jimbo la Dodoma Mjini vishkwambi 500 kwa ajili ya Shule za Msingi kumi (10) za Umma na Binafsi na kuridhika na namna ambavyo vishkwambi hivyo vimeleta mageuzi makubwa katina namna rahisi ya Ufundishaji na kuongeza uelewa mkubwa wa wanafunzi katika masuala ya Teknolojia.

Kwa mwaka huu 2018 Shirika la PROFUTURO limekubali kuongeza vishkwambi 750 pamoja na Laptops ili kwa Shule nyingine za ziada ili kusaidia kuboresha Sekta ya Elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini.




0 maoni:

Chapisha Maoni